Monday, 18 September 2017

ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO

Mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) ambao una lengo la kutatua changamoto za wakulima wadogo wadogo kufikia kuwa wakulima wa kati ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima. 
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano wa kutambulisha utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima.

 Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo  vinavyochangia katika  upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima wadogo na kutathimini mfumo wa kikanuni/ kisheria wa  udhibiti wa  pembejeo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano alisema kuwa waliamua kufanya utafiti kwa lengo la kumkomboa mkuliwa mdogo kuondokana na changamoto zinazomrudisha nyuma kimaendeleo.

“tunatekeleza mradi wa miaka miwili  unaolenga uimarishaji  utekelezaji wa  sera wezeshi za kilimo na uratibu unawezesha upatikanaji wa pembejeo (mbegu, mbolea na viuatilifu)  kudhibiti  soko na kuhamasisha upatikanaji  wake kwa wakulima wadogo” alisema Lugano

Lugano alisema kuwa utafiti ulilenga kutazama mahitaji ya pembejeo na kiwango cha usambazaji kwa kutazama aina chache za mazao, Ufanisi wa mfumo wa kudhibiti ubora wa pembejeo za kilimo na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine katika kudhibiti biashara ya pembejeo zisizo na ubora.

“Kumekuwa na malalamiko mengi yanayohusu uwepo wa mbegu na mbolea zisizo na ubora zinazowasababishia hasara kubwa wakulima wadogo wadogo ili kutatua changamoto hizo tumekuja na huu utafiti unaoweka mambo mengi wazi na jinsi gani ya kutatua kero hizo” alisema Lugano.

Aidha Lugano alisema kuwa utafiti huo umefanywa kwenye mikoa 10 ilichaguliwa kutoka katika kanda za kilimo na kuzingatia minyororo ya thamani pamoja wilaya mbili kila mkoa zilichaguliwa kwa kuzingatia umbali kutoka makao makuu ya mkoa ili kuwezesha kulinganisha uhusiano wa umbali na upatikanaji wa pembejeo.

“Mikoa ambayo tumefanya utafiti ni pamoja  Ruvuma, Kagera, Mbeya, Morogoro, Manyara, Rukwa, Iringa, Shinyanga na Simiyu hii ndio tuliona sahihi kufanyia utafiti kwakuwa ipo katika kanda za kilimo na kuzingatia minyororo ya thamani” alisema Lugano

Lugano alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora kimekuwa kikwazo moja wapo kwa wakulima wadogo wadogo hasa wale ambao hawana elimu ya kilimo na kusababisha hasa kwa wakulima na wengine kukata tamaa ya kilimo.

“Mahitaji ya mbegu kwa mwaka nchini inakadiriwa kuwa tani 120,000. Kati ya hizo, 25% (tani 30,000) huzalishwa na sekta rasmi, kiasi kinachosalia huagizwa kutoka nje ya nchi na makapuni za kibiashara” alisema Lugano

 Lugano alisema kuwa makisilio ya mahitaji na upatikanaji ya viuatilifu kwa mwaka ni changamoto kutokana na kuwa usambazaji hivyo hutegemea mahitaji mahsusi kwa eneo maalum lenye uhitaji kwa wakati maalum

“Mahitaji ya viatilifu huongozwa na Mfumo wa ‘Integrated Pesticides Management (IPM)’ Sera ya taifa ya kilimo (2013) inahimiza menejiment sahihi ya viuatilifu ambao unazingatia kanuni za kilimo bora zinazozingatia usalama na uhifadhi wa mazingira takriban viuatilifu vyote vinavyotumika nchini huagizwa kutoka nje ya nchi” alisema Lugano
 
Naye afisa kilimo wa manispaa ya Iringa Gerlad Mwamila aliupongeza utafiti uliofanywa na jukwa la kilimo la ANSAF kwa kazi kubwa waliyofanya kwa kuweza kuyafumbua maeneo yenye changamoto na jinsi gani ya kuzitatua kwa kutuwekea wazi mapendekezo yake.

"ukiangalia utafiti huu umewakusa sana wakulima na unamanufa kwa wakulima hivyo sisi viongozi ambao tupo serikalini tunapaswa kufikisha elimu hii kwa viongozi wetu wa juu pamoja na wakulima ili kukuza kilimo cha wakulima wadogo" alisema Mwamila

Mwamila alisema kuwa serikali inatakiwa kujipanga kufanikisha zoezi la upimaji ardhi ili kuwasaidia wakulima wadogo kulima kwa uhakika na sio kulima kwa kubahatisha kama ambavyo saizi wanavyolima.

"kwa kweli halmashauri zetu hazina pesa za kutosha kufanikisha zoezi la upimaji ardhi kwa wakulima wote,lakini kama halmashuri zikifanya kazi sambamba na taasisi binafsi tunaweza kufanikisha lengo la kumkomboa mkulima mdogo" alisema Mwamila

Kwa upande wake afisa kilimo wa halmashuri yawilaya ya Iringa Merry Mushi alisema kumekuwa na changamoto kwa wakulima kuuziwa pembejeo ambazo hazina ubora hivyo halmashauri imejipanga kutatua tatizo hilo.

"mara kwa mara tumekuwa tutoa elimu kwa wakulima juu ya kutumia pembejeo zisizo na ubora hivyo wakulima wameanza kuelewa na kufikisha malalamiko yake kwenye ofisi za kilimo za wilaya hiyo ni hatua kubwa sana kwetu"alisema Mushi


No comments:

Post a comment