HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 25, 2017

WENYE VIOUNGO VILIVYOKAKAMAA KUFANYIWA UPASUAJI KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN NOVEMBA 3-5 MWAKA HUU.

Meneja masoko na Mawasiliano wa Hospitali ya Aga Khan, Olayce Lotha akifafanua jambo mblele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya upasuaji wa viungo vilivyokakamaa utakao kuwa unafanyika katika hospitali ya Aga Khani jijini Dar es Salaam wajitokeze kwani matibabu hayo yatakuwa hayana gharama yeyote upasuaji utakaoaza Novemba 3hadi 5 mwaka huu. Kulia ni  Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema.
Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akiwasihi wananchi wenye matatizo ya viungo vilivyo kakamaa  wajitokeze katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa viungo ambavyo vimekakamaa kutokana na Kupata ajali za Moto, ajali za barabarani pamoja na ukatili wa Majumbani. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha  Upasuaji, Athar Ali.
Mkuu wa Operesheni wa Hospitali ya Aga Khan, Sisau Konte akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na namna wanatakavyofanya upasuaji wa Viungo vilivyokakamaa kutokana na ajali za moto pamoja na ajali za barabarani. Kulia ni  Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha  Upasuaji, Athar Ali.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

HOSPITALI ya Aga Khan  hapa nchini imeeandaa mpango maalumu kwaajili ya upasuaji wa viungo vilivyokakamaa kutokana na  ajali za moto, ajali za barabarani pamoja na ukatili naofanyika majumbani upasuaji huo utaanza Novemba 3 hadi Novemba 5 mwaka huu.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa mpango huo utaaza Novemba 3 hadi Novemba 5 mwaka huu katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaa na kwa wakazi wa Mikoani waweze kujisajili katika Hospitali yeyote ya Aga Khani na wanaoweza kusafiri na kufika katika Hospitali ya Aga Khan ya Dar es Salaam ambako kunatolewa hiyo huduma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad