HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 5 August 2017

WAZIRI LWENGE ATEMBELEA MIRADI YA MAJI YA DAWASA..

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Kazi zinazo fanyika chini ya Mradi huu ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kusambaza na kuhifadhi maji yenyeukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi milioni 6.0, ujenzi wa vituo vinne (4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa Pampu kubwa za kusukuma maji 16, ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za Umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji maji wa mabomba ya usambazaji maji mtaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilometa zipatazo 477.  
Maeneo yatakayo nufaika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kitope, Ukuni, Kerenge, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayo hudumiwa na mtambo wa Ruvu chini. Ambayo ni maeneo mengine yatakayo nufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi luisi na kiluvya, ambayo ni Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo haya huhudumiwa na mtambo wa ruvu juu ambao ulizinduliwa na mh,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Juni 21,2017.
Lengo la mradi huu ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wa kawaida , wenye viwanda na biashara katika eneo lote la mradi wanapata huduma bora za Maji hasa baada ya maji kuongezeka kufuatia kukamilika kwa upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini. Lengo lengine ni kuweka mitandao ya maji katika maeneo mengine ambayo hayakuwa na mtandao rasmi wa maji, kwa kufanya hivi mradi utawezesha maji yagawanywe kwa urahisi na uwiano zaidi.
Ili kudhibiti upotevu wa maji, mita maalum zitafungwa katika maeneo ya kupokea maji na katika matoleo ili kujuwa kiasi kamili cha maji kilicho ingia katika eneo husika na kiasi cha maji  moja kwa moja ofisi za (DAWASCO) ambapo vifaa maalum vitafungwa na itakuwa rahisi kujuwa ni wapi maji yanapotea na hivyo kuyadhibiti moja kwa moja.
Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya dola za kimarekani Milioni 32,927,222,45 kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India. 
Picha na Fadhiri Atick Michuzi Media.
Mh.waziri Lwenge akiwa katika zoezi la kukaguwa miradi ya maji ya Dawasa katika eneo la Kibamba jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi  Gerson Lwenge akipata maelezo  kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa ,Mhandisi Romanus Mwang’ingo juu ya miradi ya maji ya (DAWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majjid Mwanga akizungumza na mh.waziri na kupongeza juu ya mradi wa ujenzi wa Tenki katika Wilaya ya Bagamoyo.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad