HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 21 August 2017

WASANII NCHINI WAASWA KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF.

 Afisa habari baraza la sanaa Tanzania, Agness Kiwaga  akizungumza na wasanii kuhusu  elimu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PSPF, katika  viwanja vya Basata leo Jijini  Dar es Salaam.
 Afisa masoko mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema akizungumza na wasanii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PSPF pamoja na faida watakazozipata kupitia mfuko huo leo katika viwanja vya Basata jijini Dar es Salaam. 
 Msanii mkongwe nchini Tanzania, Stara Thomas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyopokea wito huo na kutaka wasanii wenzake kuamka na kujiunga na mifuko ya Pensheni ili kuweza kupata mikopo mbalimbali, mafao ya uzeeni, mafao ya uzazi pamoja na fao la kifo.
 Msanii Mkongwe Nkwama Badaga akizungumza na waandishi wa habari akiwataka wasanii wenzake kutumia fursa hiyo kujiunga na mfuko wa pesheni ili kujikwamua na maisha ya uzeeni na kusaidia familia.
 Baadhi ya wasanii mbalimbali wakisiliza kwa makini elimu hiyo ya kujiunga na mfuko wa pensheni ili kunufaika na maisha ya sasa na baadae kipindi watakapochoka kufanya kazi za sanaa. 
Meneja wa Bendi ya Msondongoma, Saidi Kibiriti akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa BASATA jijini Dar es Salaam  juu ya umuhimu  wa  kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwaajili ya kuhifadhi na kutunza fedha kwa ajili ya kuwasaidia maisha  ya baadae.

Na Agness Francis, Globu ya jamii.
MFUKO wa pensheni wa PSPF umewataka wasanii wote nchini kujiunga na mfuko huo ili kurahisisha maisha na kukidhi majanga yasiotarajiwa  na bila kujali wasanii walio popote nchini huduma hii kuwafikia.

hayo yamesemwa na Afisa Masoko wa mfuko wa PSPF, Magira Werema, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa licha ya kuwa wasanii hujipatia vipato kutokana na kazi zao binafsi za ubunifu  upo umuhimu wa wasanii hao kujiunga na mfuko wa pensheni  ili kuwasaidia kupata mafao ya uzeeni, Bima ya afya na fao la kifo.

Nae afisa habari baraza la sanaa Tanzania (BASATA), Agness Kiwaga, amesema kuwa wasanii wajiunge kwenye mfuko Mfuko wa Pensheni wa PSPF ili iwasaidie baade pale watakapo zeeka  kwasababu uwezo wa kufanya kazi zao utapungua hivyo basi  inakuwa ni rahisi kupata fao la uzeeni  kwaajili ya kuasaidia familia zao.

Mwana muziki Mkongwe nchini, Stara Thomas,  amesema kuwa  imezoeleka vibaya kuwa sanaa sio kama kazi zingine za taasisi kwa sasa  ipo fursa kwa wasaniii wenzake kujiunga na mfuko huo  ili kuweza kuwasaidia kupata mikopo mbalimbali.

Nae Msanii Nkwama Badanga, amesema  kujiunga na mfuko huo wa pensheni itasaidia kwa wasanii kujali na  kujituma zaidi kufanya kazi ili waweza kutimiza pesa ya mfuko ya kila mwezi ili kupata faida ya baadae na kuendelea kusaidi familia kipindi watakapochoka kufanya kazi za sanaa.

Meneja wa  bendi ya Msondongoma, Saidi Kibiriti amesema kuwa wanamuziki  wa zamani  wa muziki wa dansi  wengi wao wakishazeeka  wanakuwa na hali ngumu ya kiuchumi mpaka kufikia kuomba misaada  hii hotokana na kutokuwa na elimu kuhusu utunzaji  wa fedha  kwa ajili ya maisha ya baadae ameona umuhimui wa muamko kwa wanamuziki wenzake  kujitokeza kupata elimu ya kujiunga na mifuko ya pensheni nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad