HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 6, 2017

WANASAYANSI 200 KUONESHA KAZI ZO KUANZIA AGOSTI 8 HADI 9 KATIKA UKUMBI WA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Maonesho ya elimu ya Sayansi kwa wanafunzi wa Sekondari maharufu kwa jina la Young Scientist yanataraaji kuanza agosti 8 hadi 9 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam..

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa YST Dr Gozibert Kamugisha amesema onesho hili la aina yake litaonyesh kazi za kisayansi na ugunduzi kutoka kwa wanafunzi wa Sekondari 200 na walimu 100 kutoka mikoa yote Tanzania.

“kwa siku mbili za onesho wanasayansi Chipukizi wataonesha kazi zao katika Nyanja mbalimbali za Sayansi kama vile kemia ,fizikia , hesabu .Bilojia ,ekolojia,Sayansi ya Jamii na Teknonojia .hivyo kazi nyigi zitakazooneshwa zimejikita katika kutoa njia za kukabiliana na matatizo ya afya ,Kilimo na usalama wa matatizo ya kijamii zaidi”Amesema kamugisha.

Amesema Onesho ili limewezeshwa na udhamini endelevu wa mdhamini mkuu BG Tanzaniaa ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch ShellPlc na wadhamini wengine.

Ametaja kuwa Wanasayansi Chipukizi watakaonesha kazi nzuri watazawadiwa pesa Taslimu ,Vikombe ,Medali na Vifaa vya Maabara.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shell Afrikaa ya Mashariki n Bg Tanzaniaa,Marc den Hartog amesema kuwa wao kaama Shell wanaona fahari kubwa kuwa mdhamini wa mashindno haayo kwa kwa kufanya hivyo ndivyo wataweza kupata wanasayansi wa baada e ambao wataweza kusaidia katika uchumi wa Viwanda na sekta ya gesi na mafuta .
Mkurugenzi na muanzilishi wa Tasisi ya Young Scientist Tanzania(YST),Gozibert Kamugisha akizungumza na Waandiishi wa Habari juu ya Maonesho ya Wanasayansi Chipukizi yanayotaraji kuanza Agosti 8 mpka 9 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere,kulia ni Mkurugenzi wa Bg Tanzania ambayo ni kampuni tanzu y Royal Dutch Shell,Marc den Hartag
Mkurugenzi wa Shell Afrika Mashariki na Bg Tanzania Marc Den Hartog akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna kampuni yake inavyodhamini Maonesho hayo yenye manufa kwa kizazi cha kuwaandaa magwiji wa Sayansi nchini 
Mhasisi na Mkurugenzi wa ushauri wa Masuaala ya Kisayansi ,Joseph Clowry akizuungumza mafanikio ya tasisi hiyo ndani ya miaka sita tangu ianze kuendesha maonesho hayo.
Afisa Mahusinao ya Nje kutoka kampuni ya Bg Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch Shell,Patricia Mhondo akifafanua jambo juu ya uwekezaji wa kampuni hiyo katika kuwawzesha wanasayansi Chipukizi
Katikati ya jiji
Waandishi wa habari wakiendelea na mkutano wa Young Scientist katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo katikati ya jiji
Picha zote na Emmanuel Massaka

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad