HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 17, 2017

WANARIADHA WAPONGEZWA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA JIJINI DAR LEO.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo akizungumza wakati wa kumpongeza  Mshindi wa tatu wa Mbio za Dunia za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu pamoja na wenzake watatu ambao walienda katika mashindano ya Dunia za London Marathon nchini Uingereza.
 Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akizungumza wakati wa Jeshi la kujenga taifa limewapongeza  washindi hao walipowasili hapa nchini tangu walipotoka kwenye mashindano ya Riadha ya Dunia yaliyofanyika nchini Uingereza. Amesema kuwa "Ushindi huu si wangu peke yangu bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja."Huu ni ushindi wa wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo baadae,".
Katibu Baraza la Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja akizungumza wakati wa kuwapongeza washiriki wa mashindano ya Riadha ya Dunia ambapo Tanzania ilikuwa na wanariadha wanne na  Mshindi wa tatu wa Mbio hizo za Dunia za London Marathon kutoka Tanzania ni Alfonce Simbu.
 Mwakilishi wa Multchoice, akizungumza katika hafla fupi iliyoandali na Jeshi la Kujenga Taifa akiwapongeza washiriki wa Mashindano hapo ikiwa mshindi watatu wa mashindano ya riadha ya dunia aliibuka kidedea
Alfonce Simbu.
Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akiwa na amesimama wakati wa kutambulishwa mbele ya waalikwa waliohudhuria hafla ya kuwapongeza mara baada ya kurejea hapa nchini.
 Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza walioshiriki katika mashindano hayo ya Riadha ya Dunia.
Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akipokea  tuzo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo leo wakati wa kuwapongeza washiriki wa mashindano hayo.

 Wanariadha wakipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Jeshi la Kujenga Taifa.
 













 Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwapongeza kushiriki mashindano ya Rianda ya Dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad