HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 1 August 2017

Wagombea 20 wajitokeza kuwania urais Liberia akiwemo mchezaji bora wa dunia

 Rais wa sasa wa Liberia llen Johnson Sirleaf ambaye anamaliza muda wake mwezi October


Wagombea takribani 20 wanadaiwa kujitokeza katika kuwania kiti cha Urais nchini Liberia baada ya rais wa sasa Ellen Johnson Sirleaf kutarajiwa kustaafu baada ya kumaliza muda wake wa miaka 10 ya uongozi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, limedai miongoni mwa watu watakao wania nafasi hiyo ni mchezaji bora wa dunia wa zamani George Weah ambaye pia aliwahi kuwania katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Picha ya George Weah ambaye anatajwa kuwania urais wa Liberia October 10 mwaka huu

AFP limesema Weah atakuwa akiwania kiti hicho huku makamu wake akiwa ni Jewel Howard Taylor, 54, ambaye ni mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo Charles Taylor.
Wagombea wengine waliotajwa ni Prince Johnson, MacDella Cooper, Makamu wa sasa wa rais, Joseph Boakai na wengine. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika October 10 ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad