HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 28 August 2017

VODACOM YAANGUSHA KIAMA CHA MAGOLI 7-1 DHIDI YA HUAWEI KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI


Kikosi cha timu ya  wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ian Ferrao(katikati) aliyeshika mpira wakipozi kwenye picha kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya  kampuni ya Huawei  uliofanyika kwenye viwanjwa vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Vodacom Tanzania iliilaza Huawei  magoli 7-1.

 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Farreo (kushoto)  akimshuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei  Mengdong Gao,(kulia) akimkabidhi jezi  nahodha wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, Ngayama Matongo (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc ilishinda magoli 7-1.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Plc, Ian Ferrao (kushoto) akisaini mpira wa mfungaji bora wa mchezo wa kirafiki kati ya Vodacom na Huawei uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, ambapo Vodacom Tanzania Plc iliiadhibu Huawei magoli 7-0.Kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei  Mengdong Gao.
 Wachezaji wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakishangilia ushindi wao  baada ya kuiadhibu timu ya wafanyakazi wa Huawei mabao 7-1 wakati wa mchezo wa kirafiki ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji  hatari wa timu ya Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao akifunga goli wakati wa mchezo wa kirafiki na  Kampuni ya Huawei  uliofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.Vodacom Tanzania PLC iliibuka na ushindi wa magoli 7-1.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Farreo (jezi no.9) na  nahodha wa timu ya kampuni hiyo, Ngayama Matongo (wapili kushoto) wakishangilia ushindi  dhidi ya  timu ya kampuni ya Huawei wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc ilishinda magoli 7-1
 Mshambuliaji wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, (kushoto) Astrid Mapunda akimtoka beki wa timu ya wafanyakazi wa Huawei , wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo, uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc ilishinda magoli 7-1
 Mabeki wa timu ya Vodacom Tanzania PLC wakimdhibiti mshambuliaji wa timu ya Huawei, Li Kun , wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo, uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania iliibuka kidedea kwa magoli 7-1
 Wachezaji wa timu ya Vodacom Tanzania PLC, wakipeana mbinu za ushindi  wakati wa mapumziko ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi wa kampuni ya Huawei, uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania PLC, ilishinda magoli 7-1
Mfungaji bora wa mechi ya kirafiki kati ya Vodacom Tanzania PLC na Huawei,Kungwi Michael akionesha kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora na kikombe mara baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania, ilishinda magoli 7-1.
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Huawei Mengdong Gao (kulia)  akimkabidhi  mchezaji wa timu ya Vodacom Tanzania PLC, Kungwi Michael tuzo ya ufungaji bora  baada ya mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania, ilishinda magoli 7-1 . Kushoto ni nahodha wa timu hiyo, Ngayama Matongo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad