HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 30, 2017

Vijana kujiandikisha masomo ya Tehama yanayotolewa na Airtel na Atamizi ya DTBi



Airtel kwa kushirikian na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)  leo imetangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehema yatakayotolewa katika maabara  iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama na kuwaalika wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, wanavyuo na jamii yote kwa ujumla kujiandikisha  katika mafunzo yatakayowapatia ujuzi utakaochochea kuondoa umasikini na kukuza technolojia.

Maabara  ilianzia kama kituo cha kutoa elimu ya Tehama mwezi Julai 2017 kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama yatakayosaidia matumizi ya teknolojia na Tehama katika biashara.  Maabara hii kwa sasa itaanza kufanya kazi kwa kutoa masomo mbalimbali ambayo ni pamoja na  lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”    pamoja na  msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali ,mtandaousalama wa mtandao

Akitangaza program hizo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania , Jackson Mmbando alisema “ Tumeanzisha maabara hii ya kompyuta kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi na waalimu wa shule ya msingi  pamoja na vijana  wanaopenda kujikita kwenye masomo ya sayansi na Tehama kupata ujuzi wakiwa katika umri mdogo. Lengo letu ni kuendelea kuiwezesha sekta ya technolojia na Tehama kukua na kuzalisha vijana ambao wataweza kuvumbua na kutengeneza programu zitakazoleta suluhuhisho kwenye mahitaji ya biashara naustawi wa jamii.  Tunaamini maabara hii  ni jukwaa la kukuza vipaji vya vijana na Airtel inajisikia fahari kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi na mabadiliko haya katika jamii na nchi kwa ujumla ikiwa ni mwendelezo wa program ya Airtel Fursa inayoendeshwa na Airtel”.

Mmbando alieleza kuwa maabara hii itatoa mfunzo bure kwa walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama ila kwa  kijana yeyote asiyekua mwanafunzi au mwalimu wa shule hii atakayependa kujiandikisha ataruhusiwa kufanya hivyo.
Fomu za kujiandikisha zitapatikana kwa njia ya mtandao kwa gharama ya shilingi 20,000 kupitia www.teknohama.or.tz na  www.airtelfursa.com  au kwa kutembelea maabara  iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. Mafunzo yatatolewa  kwa wiki 4 kuanzia tarehe 4 septemba 2017.

“natoa wito kwa vijana hususani wanafunzi wa shule ya msingi kijitonyama na maeneo ya jirani kutumia fursa hii kujiendeleza zaidi”. Aliongeza Mmbando.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mhandisi George Mulamula alisema “ pamoja na kuwa na wahitimu kutoka katika vyuo mbalimbali  lakini bado Tanzania tuna uhaba wa wataalamu wabunifu wenye ujuzi  wa kutengeneza program u zitakazotatua changamoto za kijamii  za kibiashara na zinazokuza  kipato na kuondoa umasikini”

“Maabara hii  ina malengo mawili: kuwatayarisha vijana wanaotarajiwa kwenda chuo kikuu kuwa na elimu ya kibiashara ya Tehama zaidi ya kuwa na uelewa wa kompyuta na programu za simu. Lakini pili kuwaunganisha na wadau wa kibiashara ili kuwapa mwelekeo utakaowawezesha kutoa suluhisho la kiteknolojia na Tehama zitakazosaidia nchi kufikia malengo yake ya 2015 ya uchumi wa viwanda pindi watakapohitimu shule.

 DTBi inaishukuru sana Airtel na uongozi wa shule ya Msingi Kijitonyama kwa kuungana nasi na kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi haya ya Tehama kwa jamii na katika biashara kwa ujumla” alisema Mulamula
Aliongeza kwa kusema huu ni mwanzo tu kwani walimu, vijana na jamiii watapata ujuzi na ni  matumaini yetu programu hii pia itafika maeneo mbalimbali nchini.


DTBi kama msimamizi wa masomo wana timu ya wataalamu ambao wamejitolea kutoa mafunzo kwa vijana na kuleta mabadiliko katika jamii. Tunawakaribisha wale watakaopenda  kushirikiana nasi kujiunga sasa, alimalizia.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akiongea wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi). Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa DTBi.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) akiongea wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi). Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Mariam Said akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).
Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Karim Ramadhan akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad