HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 17 August 2017

Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar

Na Agness Francis,Blogu ya jamii
Katika kuelekea Tanzania ya viwanda awamu ya tano ipo fursa ya kushirikiana na nchi mbali mbali ili  kuongeza wigo katika  uchumi wa viwanda nchini.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde amesema hayo katika uzinduzi wa sita wa kokangamano  la  utafiti  barani Afrika(ARCA) kwa kushirikiana na chuo cha biashara (CBE),wakala wa vipimo (WMA) na shirika La viwango Tanzania (TBS)

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  chuo cha biashara (CBE) katika kuelezea umuhimu wa tafiti hizo  na kuleta maendeleo zaidi ya kiuchumi nchini.

Naibu Waziri Mavunde amesema kuwa serikali amewekeza fedha za kutosha  vyuoni ili kuweza kufanya utafiti na nchi mbalimbali  duniani, ili  kukuza uchumi wa viwanda na kuweza kutoa huduma bora na bidhaa bora hapa nchini.

Awali Naibu Waziri Mavunde amesema  kuwa  kuwepo kwa ongezeko la viwanda nchini itasaidia kuondoa changamoto za ajira kwa vijana na kuongeza pato la  taifa nchini.

Nae mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara  (CBE) Profesa Emanuel Mjema, amesema ili kuwa na mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali lazima kuwepo na vigezo vya kupima viwango bora ili kuweza kujua takwimu sahihi  kuwa ni watu wangapi wamepata huduma.

Hata hivyo  Mkuregenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu amesema kuwa tunajivunia nchi yetu kwa kukidhi vigezo  vya TBS na viwango bora  kulingana na  viwango   vyote  duniani.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde akifafanua jambo kwa watafiti mbalimbali barani Afrika wakati akifungua mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akikata utepe kuzindua ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA) Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akionesha ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mara baada ya kuizindua, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA)  Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.
 Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.
 Mkuregenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu akitoa mada kwa baadhi ya watafiti wa barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa sita wa watafiti hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika wakiendelea na mkutano mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad