BENKI ya NMB Tanzania imedhamini ujenzi wa duka la Nafasi Art
litakalotumiwa na watoto kujifunza mambo mbalimbali ambayo yanahusu
sanaa ili kukuza vipaji walivyonavyo vya sanaa ili watakapokua waweze
kuvitumia kutengeneza kipato.
Akizungumza wakati wa hafla
ya ufunguzi wa duka hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke alisema
udhamini huo ni sehemu ya malengo ya benki kuhakikisha inatenga pesa
ambazo zitatumika kusaidia jamii.
"Benki yetu imekuwa
ikitumia kitengo cha CSR kusaidia jamii kwa kutenga pesa kila mwaka
ambazo zinatumika kusaidia jamii, tunaamini kuwa ujenzi huu utasaidia
kuinua vipaji vya watoto ambao wanapenda sanaa ili wainue vipaji vyao,"
alisema Ineke.
Naye Mkurugenzi wa Nafasi Art Space,
Rebecca Correy aliishukuru NMB kwa uufadhili ambao wamewapa na kuwa
banda hilo litawasaidia watoto wanaopenda sanaa kuonyesha vipaji vyao
kwani kwa kipindi kirefu watoto wamekuwa wakikosa nafasi ya kushiriki
kufanya kazi mbalimbali za sanaa lakini kwa sasa wataweza kuonyesha
vipaji vyao.
Kwa upande wa mgeni rasmi kwenye halfa hiyo,
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu aliipongeza NAFASI Art
Space kwa jitihada ambazo inazifanya za kukuza sanaa nchini na kuwa
Serikali ya awamu ya tano itandelea kushirikiana nao.
No comments:
Post a Comment