HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 21, 2017

UCHANGIAJI WA MIGUU BANDIA AWAMU YA KWANZA WAANZA KWA WATU 1,000

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametangaza kuanza kwa Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwa ajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa miguu hiyo ilikuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Katika zoezi hilo Wananchi wataweza kutoa michango yao kwa njia ya Simu, huduma za Kibenki au kufika Ofisi za Mkuu wa Mkoa na kuwasilisha michango yao.

Hatua hii inakuja baada ya wenye uhitaji wa Miguu Bandia kuwa kubwa tofauti na ile iliyokusudiwa na Mkuu wa Mkoa ya watu 200 ambapo awamu ya kwanza jumla ya watu 650 walichukuliwa vipimo. Makonda amesema bado uhitaji wa Miguu hiyo ni mkubwa hivyo amewaomba wadau ikiwemo Makampuni, Taasisi na Watu Binafsi kujitokeze kuchangia ili kutimiza dhamira yake ya kuwafanya walemavu kutembea.

Hadi sasa Wadau mbalimbali ikiwemo CCBRT wamechangia Miguu 25 kwaajili ya Miguu ya watu wenye maradhi wa Kisukari,Msanii Mrisho Mpoto miguu mitatu huku Taasisi za MOI, Ajma Othopedics Medical Service wakiunga mkono zoezi hilo.

Baada ya kuona uhitaji ni mkubwa wa Wananchi Kituo cha Utangazaji cha EFM na TV E wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumzana na waandishi wa habari leo juu ya Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwaajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa Miguu hiyo
Meneja Mkuu wa EFM Radio na Tv E , Denis Busulwa (SEBO), (kulia) kizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali Tv na Radio. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad