HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 18, 2017

Uamuzi wa kesi ya bangi inayomkabili Wema Sepetu wapigwa kalenda

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, imesema uamuzi wa kupokelewa au kutokupokelewa kwa bangi iliyokutwa nyumbani kwa miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili utatolewa Septemba 12.

Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba amesema hayo leo wakati kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Katika kesi hiyo, Wema ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kete mbili za bangi na msokoto mmoja pamoja na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Akiahirisha kesi hiyo, hakimu Simba amesema, " nilitakiwa kutoa uamuzi mdogo leo kuhusiana na kielelezo kilichowasilishwa na shahidi wa upande wa mashtaka kama kipokelewe au la, lakini palitakiwa kufanya utafiti wa kutosha kutolea maamuzi, nilijipa muda mdogo sana, tumejadiliana na mawakili wa pande zote mbili na sasa uamuzi utatolewa Septemba 12 na kesi hii itaendelwa hadi  Septemba 13.

Awali ilidaiwa, February mwaka huu, katika makazi ya Wema, Kunduchi Ununio washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vyenye uzito Wa gramu 1.08

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad