HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 31 August 2017

TIMU YA PAMBA FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MBAO JUMAPILIKlabu ya Soka ya Pamba SC ya Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza inayojiandaa na ushiriki wa Ligi daraja la kwanza msimu ujao inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Mbao Fc mchezo utakaopigwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.

Mchezo huo utakua mahsusi Kwa kocha wa Pamba SC Mathias King Wandiba kujaribu wachezaji wake kabla ya Ligi daraja la kwanza kuanza septemba 16 mwaka huu ambapo licha ya mchezo huo Pamba itacheza tena michezo mingine miwili ya kirafiki itakayochezwa nje ya Mwanza.

Hali ya timu ya Pamba SC Kwa maana ya wachezaji wako katika hali nzuri kulekea mchezo huo na timu inarajia kupata ushindi baada ya kufanya mazoezi mbalimbali ikiwemo kufanya mazoezi ufukweni na mengine mengi.

Wadau na wapenzi wa Soka katika Jiji la Mwanza na maeneo yake Jirani wanaombwa kujitokeza Kwa wingi kuisapoti timu yao katika mchezo utakaopigwa jumapili hii Uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 10:00 jioni.

Imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano Pamba Sports Club

+255766527185

" PAMBA BACK TO PREMIER LEAGUE 2017/18" .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad