HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 10 August 2017

TFS Kukusanya maduhuli kieletroniki

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza utekelezaji wa ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya kielectroniki kufuatia marekebisho ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 na maelekezo ya serikali ya awamu ya tano ambao umezitaka Taasisi za serikali kujiunga na mfumo wa ukusanyaji maduhuli uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na Mipango unaoitwa Government electronic Payment Gateaway-GEPF.   
       
Akitoa ufafanuzi Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bwana Peter Mwakosya amesema Mashamba yote na ofisi za Meneja (DFM's) za Taasisi hiyo zimeunganishwa katika mfumo huo.Aidha amesema kutokana na mazingira ya vizuia(checkpoints)  kutokidhi mahitaji ya mfumo huo na hasa kushindwa kuhifadhi vitendea kazi kama kompyuta na printa kwa sasa wakala inaendelea kuunganisha kwenye mfumo vizuia vyote kwa kutumia vifaa maalum (point of sales-POS). 

  Amebainisha kwamba vifaa hivi vitatumika kukusanya maduhuli na kuhakiki uhalali wa nyaraka zinazokaguliwa katika vituo vyote vya ukaguzi wa mazao ya misitu na nyuki kwa kipindi hichi ambacho tunaendelea kuunganisha vizuia kwenye mfumo moja kwa moja. 
Bwana Mwakosya amesisitiza Maduhuli yote yanayokusanywa kwenye vizuia yanawasilishwa Ofisi ya Meneja wa Misitu wa wilaya mapema ili yaingizwe kwenye mfumo pia amewakumbusha wateja wote wa Mazao ya Misitu na nyuki kuzingatia kwamba wanatakiwa kupata hati za madai (Bill) katika mfumo kabla ya kwenda kufanya Malipo. 
Aidha amewakumbusha wateja wa bidhaa za Misitu na nyuki kwamba stakabadhi zilizokuwazinatumika kabla ya mfumo huu (ERV) hazitaendelea kutumika katika vituo vilivyounganishwa na mfumo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad