HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 16 August 2017

TECNO YAMKABIDHI JAYMONDY SIMU TOLEO JIPYA.

\
Afisa mahusiano wa TECNO Mobile Eric Mkomoya (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya WashaCheche ns kumkabidhi Raymond Msenga (Jay Mond) wa pili kutoka kushoto zawadi ya simu toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni iliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya simu za TECNO imemzawadia zawadi ya simu mchekeshaji Raymond Msenga maarufu kama JayMondy ikiwa ni toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni aliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo Eric Mkomoya alisema “nia na madhumuni ya kampuni yetu ni kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania kupitia simu hii mpya, vijana wanaotaka kufanikiwa wanapitia vikwazo vingi, ila Tecno inataka kuwasaidia kupitia washa cheche.”

Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni aliomba simu kutoka Tecno Mobile kupitia video zake ili aweze kurekodi kwa ubora mzuri. Tecno Mobile walisikia kilio chake na kumpa zawadi ya simu mwaka mzima kwa kila toleo.

“Nimefurahi kupata zawadi ya simu hii, na kikubwa na ni nafasi ya kupata mfululizo wa matoleo yote mapya ya simu zao, nawasihii vijana wenzangu wenye vipaji wawashe cheche zao na wanaweza kupata msaada kutoka Tecno Mobile.” Alisema Raymond Msenga maarufu kama Jaymond.

Meneja wa masoko mitandaoni wa TECNO, Kelvin Boniface alisema “Namna ya kushiriki katika kampeni hii ni rahisi, Upload video au picha Kwenye mitandao ya kijamii ukitumia hashtag #WashaCheche bila kusahau kutuTag “Tecno Mobile Tanzania kwenye mitandao yetu ya kijamii ya twitter, Facebook na Instagram” alisema

Kampeni hii itasukumwa na simu yao mpya aina ya TECNO SPARK (TECNO CHECHE) ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiletea maendeleo na kujikwamua kimaisha.

Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni akikabidhiwa simu na meneja wa masoko mtandaoni Chen Bo simu mpya aina ya TECNO SPARK.

Afisa mahusiano wa TECNO Mobile Eric Mkomoya akiwaonyesha waandishi wa habari toleo jipya la simu zao kabla ya kumkabidhi Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad