HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 15 August 2017

TAASISI YA WAJIBU YAZINDUA RIPOTI YA RIPOTI CAG

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Taasisi ya Wajibu imezindua Ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016 katika maeneo ambayo ni muhimu kwa kila mtanzania kuweza kujua ripoti hiyo kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa. 
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kabla ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo, Lodovick Utouh amesema kuwa ripoti hiyo imeangalia maeneo matatu ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016  ambayo  ni Serikali Kuu, serikali za Mitaa pamoja na Mashirika ya Umma.
Amesema kuwa katika ripoti hiyo kwa deni la taifa linatakiwa kwa serikali kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kulipa na shughuli zingine za maendeleo ziendelee bila kuongeza mapato na kulipa deni kutafanya shughuli hizo za maendeleo kukwama.
Utouh amesema katika ripoti hiyo agizo la serikali kwa Halmashauri kutenga asilimia 10 ya kuwawezesha vijana na wanawake inatakiwa kuwa ni mikopo wanayopata inatakwa kuwa katika mzunguko na  kuweza kila mtu kumfikia mkopo huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesababu za serikali na maoni yake iliyoangalia maeneo matatu ya ripoti hiyo leo.
 Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya Taasisi ya  wajibu. 
 Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizindua ripoti ya taasisi ya wajibu  leo jijini Dar es Salaam.
Picha pamoja Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert, Watendaji wa Taasisi ya wajibu pamoja na wadau mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad