Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango
Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa
kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support
(THPS). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Wageni
na wafanyakazi wa taasisi ya THPS waliohudhuria katika Uzinduzi wa
Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao
utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health
Promotion Support (THPS). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Tanzania Health
Promotion Support (THPS) Dkt. Augustine Massawe akizungumza katika
uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano
ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016- 2020. Tukio hilo lilifanyika
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt.
Redempta Mbatia akizungumza juu ya uzinduzi wa Mpango Mkakati ya
kusaidia mifumo ya afya na kuelezea malengo ya taasisi hiyo kwa miaka
ijayo kati ya mwaka 2016-2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es
Salaam.
Mmoja ya vijana waelimisha Rika kutoka Zanzibara akitoa somo jinsi ya kujitambua.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya),
Dkt. Mpoki Ulisubisya akizindua Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia
mifumo ya afya wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS)
ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia na wadau wengine. Tukio
hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya),
Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa nne toka Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia (wa tako kutoka kushoto) pamoja na
wadau wa afya wakionyesha chapisho la Mpango Mkakati wa kwanza wa
kusaidia mifumo ya afya wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support
(THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Health Promotion Support
(THPS) inayosaidia Wizara za afya Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga
ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huduma, matibabu na msaada kwa kuimarisha
mifumo ya afya imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka
mitano.
Akizungumza katika uzinduzi
huo wa mpango mkakati uliofanyika Jijini Dar es salaam leo. Mwanzilishi
na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dkt. Augustine Massawe alisema mpango
mkakati wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016
mpaka 2020 umelenga kusaidia juhudi za Wizara ya afya, Serikali za
mitaa, Washiriki wengine na Wadau kuhakikisha huduma bora za afya
zinazoshugulikia afya ya umma ikiwemo magonjwa yanayoambukizwa na
yasiyoambukizwa ili kuboresha matokeo ya afya kiujumla katika jamii.
Dkt.
Massawe alisema anatarajia mpango mkakati utazingatia mawazo kati ya
wadau muhimu wa THPS na kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri.
“tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuathiri ubora wa huduma
za afya na kujenga taifa huru la VVU/UKIMWI. Nina matumaini kuwa mpango
mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi
katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na rasilimali, kuimarisha
shughuli mbalimbali na kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine
wanafanya kazi kwa malengo.
Akizungumzia juu ya
uzinduzi wa mpango mkakati, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta
Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo ni kutazamia mbali
VVU/ UKIMWI na kushughulika na magonjwa mengine yenye vitisho katika
jamii, kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza
ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake.
“Mpango
mkakati huu umekuja wakati muafaka ili kuhakikisha tunafikia idadi
kubwa ya watu wenye mahitaji, wakati huo huo tukikuza na kuendeleza
taasisi. Tunataka kuendelea kuzingatia maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na
huduma bora za afya, uwezo endelevu wa kifedha, utawala bora na
uwajibikaji wa pamoja na wafanyakazi wenye uwezo na kujitolea. Kama
taasisi mpya nchini Tanzania tunathamini sana Imani, msaada na fursa ya
kutumikia watanzania inayotolewa na serikali kuu, serikali za mtaa,
wafadhili, washirika watekejezaji na wadau wengine muhimu kutoka pande
zote mbili za jamhuri. Mwisho kabla ya kumaliza tunashukuru kwa msaada
endelevu wa kifedha na kiufundi kutoka kwa wafadhili wetu: Watu wa
Marekani kupitia PEPFAR/ CDC na taasisi ya taifa ya afya Marekani (NHI) ,
UNAIDS , Chuo kikuu cha Harvard, Chuo kikuu cha Colombia na taasisi ya
mfuko wa uwekezaji kwa watoto uliopo Uingereza”.
Aidha
Dkt. Mbatia alisisitiza kuwa mwelekeo wa mpango mkakati kwa miaka
mitano ni kufaidika kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja
kwa mamilioni ya Watanzania. Mpango huo umesimama kama nguzo ya kuongeza
na kubuni ufumbuzi wa afya bora ya kupambana na VVU na UKIMWI, mifumo
ya utoaji afya na changamoto nyingine za afya zinazoathiri Watanzania.
No comments:
Post a Comment