
Msaidizi wa Meneja anayeshughulikia Maendeleo ya Shamba Bwana Salum Yakuti amesema wameamua kuifanyia majaribio Teknolojia hiyo kwa sababu Mahitaji ya Mazao ya Misitu amekuwa makubwa ukilinganisha na Upandaji Miti.
Amezitaja faida za kutumia kikonyo kwamba mti una kuwa hauathiriki na magonjwa, miti inatoa mazao yenye ubora sawa na kwa sababu miti hiyo inakuwa kwa haraka itapelekea kufikia mahitaji ya watumiaji kwa muda mfupi.
Akijibu swali la Mh. Chunga wa Bunge la Malawi Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi ambaye alitaka kufahamu ni nini kinafanya mti huo ukue kwa haraka Bw. Yakuti alisema kwa ufupi kwamba wanakata kitawi kidogo cha mti, wanaweka kwenye homoni inayosaidia mti huo kuota kwa haraka.

Majaribio ya upanndaji miti kiteknolojia kupunguza muda
No comments:
Post a Comment