HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 18 August 2017

Picha: Jeshi la Kujenga Taifa lampa tuzo Alphonce Simbu

Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo akizungumza wakati wa kumpongeza Mshindi wa tatu wa Mbio za Dunia za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu pamoja na wenzake watatu ambao walienda katika mashindano ya Dunia za London Marathon nchini Uingereza.
 Alphonce Simbu akipokea tuzo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo kama pongezi kwa ushindi wake.
Mshindi wa Medali ya Shaba katika mbio za dunia za London, Alphonce Felix Simbu pamoja na wenzake wamepongezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kuiwakilisha nchi vyema katika michuano ya riadha ya dunia ya London nchini Uingereza.
Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akizungumza wakati wa Jeshi la kujenga taifa limewapongeza washindi hao walipowasili hapa nchini tangu walipotoka kwenye mashindano ya Riadha ya Dunia yaliyofanyika nchini Uingereza. Amesema kuwa "Ushindi huu si wangu peke yangu bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja."Huu ni ushindi wa wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo baadae,".
Simbu alifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mashindano hayo na kupata Medali ya shaba
Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akiwa na amesimama wakati wa kutambulishwa mbele ya waalikwa waliohudhuria hafla ya kuwapongeza mara baada ya kurejea hapa nchini.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba pamoja na wanaridha wenzake katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 a jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwapongeza kushiriki mashindano ya Rianda ya Dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad