Afisa Muuguzi Mwandamizi, Gudila Mambacho (kushoto) wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) akichukua vipimo vya presha toka kwa mmoja wa
wananchi (kulia) waliojitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa
na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa
Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi
aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha
Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma
mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku
ya wakunga duniani.
Muuguzi mwandamizi na afisa lishe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Dotto Msabila Kafulie (kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi
aliyejitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha
Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya
udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Maofisa Wauguzi na wataalam wa Kisukari Swaumu Gulumo
na Sarah Mwakilima wakimuhudumia mmoja wa wananchi (kushoto)
waliojitokeza kupima magonjwa mbalimbali bure katika kongamano la Chama
cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa
ni maadhimisho ya siku ya wakunga duniani.
Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi
aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha
Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma
mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku
ya wakunga duniani.
Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (aliyeshika kipaza sauti)
akizungumzia huduma mbalimbali ya NMB kwa baadhi ya wananchi
waliojitokeza kupata huduma anuai za afya bure zilizokuwa zikitolewa na
Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili
chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam, ikiwa ni
shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani.
Afisa Muuguzi Mwandamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Janeth
Mwambona (kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi aliyejitokeza kupata
huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA)
Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya
NMB jijini Dar es Salaam.
CHAMA
cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini
ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB kimetoa huduma za afya mbalimbali bure
jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya
wakunga duniani.
Akizungumza leo na mwandishi wa habari hizi katika tukio hilo
linaloendelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jirani na jengo la watoto,
Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wakunga Tanzania tawi la Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Bi. Elizabeth Thawe aliwataka wananchi kujitokeza
katika eneo hilo ili kuweza kupata huduma hizo za afya bure.
Alisema
huduma wanazotoa bure siku nzima ya leo ni pamoja saratani ya shingo ya
kizazi, saratani ya matiti, elimu kuhusu lishe bora, shinikizo la damu
(BP), sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji watoto kwa akinamama.
"Kuelekea maadhimisho ya siku yetu, tumejitolea kupima afya bure kwa
wananchi wote watakaojitokeza katika eneo hili...huduma zinazotolewa
bure leo ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti,
tunatoa elimu kuhusu lishe bora, tunapima shinikizo la damu (BP),
tunapima sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji,
"
alisema Bi. Elizabeth Thawe.
Aliongeza kuwa huduma hizo zinatolewa kwa wanachama wa Chama cha Wakunga
Tanzania (TAMA) tawi la Muhimbili kwa kushirikiana na wengine kutoka
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Mifupa Muhimbili
(MOI) pamoja na vyuo vyote vya afya vinavyozunguka Hospitali ya
Muhimbili.
Alisema mbali na kutoa huduma hizo bure siku ya pili ya maadhimisho
(yaani Agosti 7, 2017) watafanya kongamano la kisayansi katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku
hiyo muhimu kwa wakunga.
Aidha
aliishukuru Benki ya NMB ambayo ni wadhamini wa kuu wa maadhimisho hayo
pamoja na makampuni mengine yaliojitokeza kusaidia kufanikisha shughuli
hizo.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia misululu ya wananchi waliojitokeza
kupata huduma za afya bure eneo hilo na wengine kuvutiwa na huduma za
NMB zilizotolewa eneo hilo, kuwaunganisha wananchi na huduma za kibenki.
Maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) wakimfungulia akaunti mmoja wa
wateja (kulia) aliyejitokeza kupata huduma hizo katika kongamano la
Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili
ambapo mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata
huduma mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya
siku ya wakunga duniani.
Sehemu ya wananchi wakiwa katika foleni kupata huduma za afya bure
zilizokuwa zinatolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la
Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
No comments:
Post a Comment