HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 21 August 2017

NGAO YA JAMII SASA KUPIGWA SAA 11 ALASIRI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewatangaza waamuzi watakaochezesha  mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba utakaopigwa siku ya Jumatano kuanzia saa 11 jioni katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo wa ufunguzi wa ligi unatarajiwa kuchezeshwa na Mwamuzi Bora wa msimu wa 2016/17 Hery Sasii kutoka Dar es salaam akisaidiwa na Ferdinand Chacha  wa Arusha pamoja Hellen Mduma wa Dar es salaam.

Pamoja na hilo, TFF imemzuia  kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano.


Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba, Chirwa hawezi kucheza kesho kwa sababu katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC alimsukuma refa mjini Mwanza.

“Chirwa atakukosa mchezo wa Jumatano dhidi ya Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa saa 11:00 mjini Dar es Salaam kutokana na kesi inayomkabili ya kumsukuma mwamuzi aliyechezesha mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC,”alisema.

Lucas amesema mshambuliaji aliyejiunga na Yanga msimu uliopita kutoka PF Platinums ya Zimbabwe amesema atalazimika kuendelea kuwa nje hadi hapo Kamati ya Masaa 72 itakapokutana na kutoa maamuzi dhidi yake.

Viingilio katika mchezo huo ni Sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, 10,000 Viti vya Orange, 20,000 kwa VIP B ba 25 kwa VIP A .6/17 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad