HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 10 August 2017

MWANAMKE ACHINJWA KWA MGANGA WA KIENYEJI MKOANI DODOMA

Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mariam Saidi mkazi wa Kigoma aliyeuwawa kwa kuchinjwa na kisha kichwa na baadhi ya viongo vyake  kuchomwa moto katika kijiji cha Chamwino Ikulu wilayani Chamwino.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi Mwandamizi Lazaro Mambosasa anasema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 8 mwezi huu katika kitongoji cha Chang'ombe kijijini hapo ambapo mwili huo ulikutwa nyumbani kwa mganga wa kienyeji aliyetambulika kwa jina la Ashura Mkasanga Matha huku sura ikishindwa kutambulika baada ya kichwa kuchomwa moto.

Kamanda Mambosasa anasema mganga huyo wa jadi asiye na kibali cha kuendesha shughuli za tiba asili pia amekutwa  akilaza wagonjwa nyumbani kwake kufanya matambiko  kupiga ramli chonganishi na tohara za watoto ambapo watu wanane waliokutwa wamelazwa pamoja na mume wa mganga huyo Noel Mazengo na msaidizi wake Victor Chibelenje wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Katika tukio jingine mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Masumbuko Nyerere amefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakati akichimba mchanga kiholela katika kijiji cha Ntyuka manispaa ya Dodoma ambapo kamanda Mambosasa amewataka maofisa wa idara ya madini na mazingira kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika machimbo pamoja na kutoa elimu ya uchimbaji salama.

Chanzo: ITV Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad