HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 11, 2017

MTUHUMIWA SHOSE SINARE ALALAMIKIA WAPELELEZI WA KESI YAO.

 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Miss Tanzania, Shose  Sinare ameuomba upande wa mashitaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, pamoja na wenzake wawili walete  mawasiliano yanayofanyika kati ya Tanzania na Uingereza juu ya upelelezi dhidi ya kesi yao.

Shose amedai hivyo leo katika  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha, Mbali na Sinare, washitakiwa wengine ni   katika kesi hiyo ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Msamire Kitilya, na Sioi Solomon.

Sinare alidai  kuwa mpaka sasa wamekaa gerezani kwa zaidi ya mwaka na nusu hivyo upande wa mashitaka uwasilishe mawasiliano hayo.
Mapema, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliieleza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika kwani bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi huo.

Kufuatia hayo, Hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25 mwaka huu ili upande wa mashitaka ueleze muendelezo wa kile kilichowasilishwa kortini. Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550  kwa  serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Agosti 2, 2012 Sinare kwenye  Makao Makuu ya benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni kwa  nia ya kudanganya aliandaa nyaraka  ya pendekezo akijaribu kuonyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stabic  ya Tanzania  watatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni  550 kwa serikali  ya Tanzania  kwa ada ya uwezeshaji ya asilimia 2.4 ya kiasi cha mkopo huo wakati akijua kuwa sio kweli.

Inadaiwa kuwa  Agosti 2, 2012 ,Sinare alitoa nyaraka za uongo za mapendekezo ya kuonyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stabic  ya Tanzania,  watatoa mkopo wa dola za kimarekani  milioni 550 na kuziwasilisha katika ofisi za Wizara ya fedha  wakati akijua kuwa sio kweli.

Aliendelea kudaiwa kuwa  Septemba 20, 2012 katika  Makao Makuu ya Benki ya Stanbic nchini yaliyopo Kinondoni, alitenda kosa la kughushi barua.
Sinare anadaiwa kughushi barua ya mapendekezo ikionyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stabic  ya Tanzania  watatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 550 kwa Serikali  ya Tanzania  kama ada ya uwezeshaji wa asilimia 2.4 ya kiasi cha mkopo huo wakati akijua kuwa sio kweli.

 Agosti 21,2012,  Sinare anadaiwa kuwa kwa lengo la kulaghai aliwasilisha nyaraka hizo za uongo kuiwezesha Serikali ya Tanzania kupata mkopo huo wa kiasi hicho cha ada ya uwezeshaji, katika ofisi za Wizara ya Fedha.

Washtakiwa hao kwa pamoja  wanadaiwa kughushi nyaraka za makubaliano  kwamba  Novemba 5 ,2012 katika benki ya Stanbic makao makuu Kinondoni  Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya walighushi waraka wa makubaliano wa Novemba 5, 2012.

 Inadaiwa kuwa waraka huo ulikusudia kuonesha kuwa Stanbic Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano  na kampuni ya Enterpirise Growth Market Advisors  (Egma) Limited kuwezesha upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 550  kwa ajili Serikali ya Tanzania .

Wanadaiwa kuwa  Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo  na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma T Ltd. Washtakiwa  hao wanadaiwa  kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani milioni sita  katika akaunti tofauti tofauti  za benki.

Kati ya  Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa  kuwa waliweka pesa hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu kuwa pesa hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad