MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhiwa mradi wa
Maboresho ya Mtaa Samora uliogharimu zaidi ya Shilingi Milion 840
zilizofadhidhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la
maendeleo Japan (JAICA) na Manispaa ya Ilaa uliokamilika kwa 100%.
Mradi
huo umehusisha ujenzi wa sehemu za Maegesho, mapumziko ya watu,upandaji
wa miti na Maua, maboresho ya mazingira, uwekaji wa alama za barabarani
pamoja na maboresho ya mitaa kuanzia Makutano ya Barabara ya Samora na
Morogoro ikienda sambamba na kupunguza msongamano.
Akizungumza
kwenye makabidhiano hayo Makonda amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Sophia Mjema kuhakikisha majengo yote ya Gorofa eneo la Posta yanafungwa
Taa na Runinga za Matangazo ili kupendezesha Mji na kuongeza mwanga
nyakati za usiku.
Amesema
katika nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani majengo marefu yamekuwa
sehemu ya matangazo hususani nyakati za usiku na kufanya miji kupendeza
hivyo hata Dar es salaam tunaweza kufanya hivyo ili kufikia azma ya Rais
Magufuli kutaka Dar es salaam kuwa mji wa Biashara.
Aidha
amesema mradi huo utakuwa wa awamu ili kuhakikisha mitaa na maeneo ya
wazi yanaboreshwa ilikuwafanya wananchi kuwa na maeneo mengi ya
kupumzika na kubadilishana mawazo ikiwa ni maono yake ya Dar es salaam
Mpya.
Awali
eneo hilo lililofahamika kama Kaburi Moja lilikuwa likitumika kama
Choo, Maegesho holela na wakati mwingine likitumiwa kwa uhalifu na
uchafu wa mazingira.
Amewataka
wananchi kutunza vizuri eneo hilo ili liweze kuwanufaisha wengi huku
akipiga marufuku wamachinga kutofanya biashara kwenye eneo hilo.
Aidha
Makonda amesema anataka kuona vituo vyote vya Daladala mkoa wa Dar es
salaam vinaboreshwe kuwa vya kisasa na kuwa sehemu ya matangazo ili
kupendezesha mji na kuchangia ongezeko la mapato.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kushirikiana na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Isaya
Mwita Charles wakikata utepe kuzindua mradi huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na katika hafla ya
makabidhiano mradi wa Maboresho ya Mtaa wa Samora uliogharimu zaidi ya
Shilingi Milion 840 zilizofadhidhiliwa na Serikali ya Japan kupitia
Shirika la Kimataifa la maendeleo Japan (JAICA) leo jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Isaya
Mwita Charles akikangua mradi wa Maboresho ya Mtaa Samora uliogharimu
zaidi ya Shilingi Milion 840 zilizofadhidhiliwa na Serikali ya Japan
kupitia Shirika la Kimataifa la maendeleo Japan (JAICA).
No comments:
Post a Comment