HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 15, 2017

MFANYABIASHARA wa Kariakoo kizimbani kwa kukamatwa na sare za jeshi la wananchi.

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MFANYABIASHARA wa Kariakoo, Casto Onyomolile Ngogo (35) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya kukutwa na sare mbalimbali za Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ.

Mshtakiwa huyo ambaye amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba anashtakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai Juni 15, 2017 mshtakiwa huyo anayeishi Tabata Segerea, alikutwa na Suruali 5000 za JWTZ zenye thamani ya milioni 50.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kukutwa na vifaa hivyo katika maeneo ya bandari kavu ya Galco Inland Container (ICD) iliyopo Sokota Chang'ombe.

Pia mshtakiwa huyo alikutwa na alikutwa na maofisa wa polisi akiwa na tisheti 50 za JWTZ zenye thamani ya Sh 500, 000 pia Juni 17, mwaka huu huko African Inland Container Deport mshtakiwa alikutwa na polisi akiwa na pea 20 za viatu vya JWTZ bila ya kuwa na uhalali.

Mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Pia (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana chini ya kifungu cha 36 (2) cha sheria ya uhujumu uchumi. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 29,mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad