HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 29, 2017

MBAO FC YAJAZWA MILION 140 YA UDHAMINI NA KAMPUNI YA GF TRUCKS & EQUIPMENT LTD

Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali  na  Mwenyekiti wa Mbao Fc Solly Zephania Njashi wakionyesha hati ya makubaliano ya Mkataba  ikiwa ni mkataba wa udhamini wa timu hiyo kwa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 140 sambamba na basi la wachezaji.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

UONGOZI wa klabu ya Mbao Fc umeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya milioni 149 na kampuni ya GF Trucks & Equipments ikiwa ni udhamini wa timu hiyo kutoka Jijini Mwanza.

Kampuni hiyo imeridhishwa na maendeleo ya timu hiyo na kuamua kuwapatia udhamini kwani hawajawahi kushiriki katika udhamin i wa soka la Kiwango cha ligi kuu.

Mkataba huo uliosainiwa mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Imrani Karmali amesema kuwa mkataba huo ni wa kihistoria kwani unaenda kuleta na kukuza  maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Karmal amesema kuwa, madhumuni makubwa ni kukuza vipaji vya mpira wa miguu na wanatarajiwa kuisaidia Mbao Fc kufikia malengo yao msimu huu, " tunafahamu usafiri umekuwa ni tatizo kwa klabu nyingi ndogo za Ligi Kuu na hicho kimetupelekea kuanza na basi msimu huu ambapo katika mkataba wa milioni 140 utajumuisha sambamba na basi hilo la wachezaji lenye thamani ya milioni 70,".

"uwezo waliouonesha katika ligi kuu na hata kuingia fainali ya kombe la FA ulituhamasisha kuifuatilia kwa ukaribu sana  na tuna imani kwa msaada wetu Mbao itaendelea kufanya vizuri na si hao tu bali hata ajira kwa vijana zitaongezeka,"amesema Karmali.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mbao Fc, Solly Zephania Njashi ameusifu mkataba huo na kusema kuwa utazidi kuleta chachu ya maendeleo katika klabu yao na hata kupunguza gharama za mahitaji kwa wachezaji.

Njashi ameishukurui kampuni ya  GF Trucks & Equipments  kwa mkataba huo na kuwaahidi mashabiki na wapenzi wa Mbao kuwa mwaka huu wataendelea kufanya vizuri na kuendelea kusalia katika Ligi kuu msimu ujao.

 Baada ya kusaini mkataba huo, kampuni ya  GF Trucks & Equipments i iliwakabidhi mfano wa jezi zitakazovaliwa na timu ya Mbao tayari zikiwa zimeshaweka nembo ya kamouni hiyo.
 Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia makubaliano ya udhamini wa mkatabwa mwaka mmoja na na kampuni ya GF Trucks & Equipments wenye thamani ya Milioni 140, kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali 
 Afisa Masoko wa Kampuni ya  GF Trucks & Equipments Kulwa Bundala akizungumza na wanahabari baada ya kuingia mkataba na timu ya Mbao Fc wenye thamani ya Milioni 140 kwa mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali  na  Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi wakionyesha jezi za Mbao zitakazotumikia mwaka huu.


\

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad