HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 11 August 2017

MANAHODHA WA MCHENGA NA TMT WATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WA MAKONGO.


Nahodha wa Mchenga Mohamed Yusuph (kushoto) pamoja na Nahodha wa TMT (kulia) wakikabidhi mipira kwa viongozi wa timu ya mpira wa kikapu ya Sekondari ya Makongo walipowatembelea jana na kuwahamisha kushiriki michezo mashuleni na kuirejesha heshima ya mchezo wa mpira wa kikapu

Na Zainab Nyamka, GlobU ya Jamii.

Katika kukuza na kurejesha heshima ya mpira wa kikapu nchini, waandaaji wa michuano ya Sprite Bball Kings 2017 wamewahamasisha wanafunzi kuupenda na kuuthamini mchezo huo kwani elimu na michezo inaenda sambamba.

Hayo yamesemwa na Manahodha wa timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings inayoendelea wikiendi hii wakati akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari Makongo.

Nahodha wa timu ya Mchenga Bball Stars, Mohamed Yusuph amesema kuwa masomo na elimu yanaenda sambamba hivyo wanafunzi wasiwe waoga kuonesha vipaji vyao mbele ya jamii kwani wanaweza kupata nafasi za masomo kupitia mchezo wa mpira wa kikapu.

"Wanafunzi wanatakiwa kuonesha vipaji vyao kwani wasione kama watashindwa kufanya vizuri katika masomo yao, kwa ufupi elimu na michezo vinaenda sambamba," amesema Yusuph.

Aidha Yusuph amewataka wanafunzi kujiunga na timu za mpira wa kikapu kwa ajili ya kuweza kucheza mchezo huo na zaidi katika timu yao ya Mchenga kuna timu za vijana kuanzia miaka 13 na wengine wapo katika timu za taifa.

Kwa upande wa Nahodha TMT, Isihaka Masoud amewataka wanafunzi kuithamin na kuipenda michezo kwani michezo ni afya na wakipata wasaa wa kupumzika wasiache kujumuika na wenzao katika mchezo wowote.

Baada ya kumaliza kuongea na wanafunzi, manahodha hao walitoa zawadi ya mipira kutoka Sprite na t-shirt kwa uongozi wa timu ya mpira wa kikapu ikiwa ni katika kuongeza chachu ya kucheza mpira wa kikapu na kurejesha heshima ya mchezo huo.

Nahodha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya Mchenga Mohamed Yusuph akizungumza na wanafunzi wa Sekondari Makongo na kuwahamisha kujikita katika mchezo wa mpira wa kikapu na zaidi elimu na michezo vinaenda sambamba na baadae kuwakabidhi zawadi mipira na t-shirt kutoka Sprite.

Nahodha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya Mchenga Mohamed Yusuph akiwa na mwanafunzi wa Makongo akijaribu kumtoka na mpira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad