HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 19 August 2017

M-KOPA YAFUNGA UMEME JUA WENYE THAMANI YA Tshs 4,959,000. KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWINYI MKURANGA PWANI

--
 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi boksi la Vifaa vya umeme wa jua kma ishara ya makabidhiano ya mradi wa umeme uliojengwa katika shule ya Sekondari ya Mwinyi Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kamati ya shule iliyoongozwa na Mwalimu Mkuu Martin Chuwa Mtendaji kata .Juma Difa na Afisa Elimu Iddi Mdoe
 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi zawadi kwa Mtendaji kata .Juma Difa mara baada ya kukabidhi mradi wa Umeme jua katika shule ya Sekondari ya Mwinyi

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kampuni ya vifaa nishati jadidifu vya Jua ya M-Kopa imefunga vifaa vya Umeme jua katika Shule ya Sekondari  ya Mwinyi iliyoko Mkuranga mkoa wa Pwani vyenye thamani ya shilingi Tshs 4,959,000.

akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja Msaidizi wa kampuni ya M-Kopa Nchini, June Muli amesema kuwa wameameamua kutoa msaada huo ka sehemu yao ya kurudisha wanachokipata kwa jamii hivyo waliona matatizo ya shule zisizokuwa na Umeme.

"Kuna Changamoto kubwa sana ya kusoma katika shule amabzo azina umeme hali inayofanya wanafunzi wanaochukua masomo ya Sayansi kushindwa kuifunza vizuri katika maabara zao na hata wakati wa usiku kuhsindwa kujisomea hivyo sisi kama M-Kopa tumeweza kuchangia upatikanaji wa vifaa hivi mpka kuahakisha umeme unawaka shuileni hapa tunamini sasa vijana wetu wataweza kujifunza na kufaulu vizuri"amesema June Muli.

ameongeza kuwa katika tafiti yao kwa wazazi wamebaini kuwa asilimia 92% ya watoto wanaosoma katika shule zenye umeme ufanya vizuri Darasani kuliko wale wanaosoma kwenye giza .

kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwinyi ,Martin Chuwa amewashukuru kampuni hiyo kwa kuweza kutoa Msaada huo ambao utasaidia kuinua taaluma ya shule hivyo na kusema kuwa anawashukuru kwa kuchagua shule hiyo kuwa ya kwanza kufikiwa na mradi huo ambao unalengo la kuboresha elimu nchini  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad