HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 8 August 2017

KAMA ULIPITWA NA MECHI YA SIMBA DAY, BASI HUU MTIRIRIKO WA PICHA UTAKUFAAA

Wacheza shoo wa Bendi ya Twanga Pepeta wakiwa wamembeba juu juu Msemaji machachari wa timu ya Simba, Haji Manara wakati wa Sherehe za Simba Day zilizofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. Ambapo Timu ya Simba iliwakaribisha wageni wao Rayon Sports ya Rwanda kwa mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa Simba kutoka kifua mbele kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0. nimekuwekea mtiririko wa picha za shughuli hayo hapo chini hivyo endelea kufurahia.
 Mabeki wa timu ya Simba, Jonas Mkude (kulia) na Mzamiru Yassin wakichuana na Mshambuliji wa Timu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda, katika mchezo wa kujipima nguvu ikiwa ni sehemu ya Sherehe za kuadhimisha miaka 81 toka kuanzishwa kwa timu hiyo, zinazofahamika kama Simba Day. Mchezo huo umemalizika jioni hii katika dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 1-0 .
 Beki wa Timu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda akionyesha umahiri wake wa kuondosha mpira wa hatari langoni mwake, katika mchezo wa kujipima nguvu ikiwa ni sehemu ya Sherehe za kuadhimisha miaka 81 toka kuanzishwa kwa timu hiyo, zinazofahamika kama Simba Day. Mchezo huo umemalizika jioni hii katika dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 1-0 .
 Mshambuliaji mpya wa Timu ya Simba, John Bocco akiwa na mpira mbele ya mabeki wa timu ya  Rayon Sports ya nchini Rwanda, katika mchezo wa kujipima nguvu ikiwa ni sehemu ya Sherehe za kuadhimisha miaka 81 toka kuanzishwa kwa timu hiyo, zinazofahamika kama Simba Day. Mchezo huo umemalizika jioni hii katika dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 1-0 .
  Mshambuliaji mpya wa Timu ya Simba, Emmanuel Okwi akiondoka na mpira mbele ya mabeki wa timu ya  Rayon Sports ya nchini Rwanda, katika mchezo wa kujipima nguvu ikiwa ni sehemu ya Sherehe za kuadhimisha miaka 81 toka kuanzishwa kwa timu hiyo, zinazofahamika kama Simba Day. Mchezo huo umemalizika jioni hii katika dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 1-0 .
 Mgeni rasmi katika mchezo wa kujipima nguvu kati ya Timu ya Simba na Rayon Sports ya Rwanda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, January Makamba (kushoto) akimuandalia, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wakati akisalimiana na wachezaji wa timu hizo kabla kuanza kwa mechi hiyo. mwenye kaptula ni Mdhamini wa Simba, Mohamed Dewji "Mo".
 Kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.
Kikosi cha Simba.


 Kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.
Kikosi cha Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad