HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 3 August 2017

IDARA YA UHAMIAJI:MGOMBEA URAIS WA TFF WALLACE KARIA NI RAIA HALALI WA TANZANIA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Idara ya Uhamiaji Nchini imethibitisha kuwa  Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace John Karia ambaye ni Mgombea Urais wa TFF  katika uchaguzi unatarajia kufanyika August 12  mwaka huu ni Raia halali wa Tanzania.
 Akizungumza na waandishi habari leo makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Msemaji Mkuu wa Idara hiyo  Ally Mtanga amesema kuwa mmoja wa wagombea wa Urais wa TFF alimkatia rufaa mgombea mwenzake Wallace Karia kuwa si raia wa Tanzania .
 "Wallace Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357(Rejeo la 2002) na kanuni zake, wakati huo huo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi"
Mtanga amesisitiza  utambuzi wa uraia upo kisheria sura ya 357 (rejeo la 2002) uraia hauangaliwi Rangi, kabila wala dini.
 Idara hiyo imevitaka vilabu vyote na taasisi za michezo kuhakikisha wafanyakazi wote na wachezaji ambao raia wa kigeni wanatimiza taratibu zote za kisheria za kukaa nchini  bila kufanya hivyo sheria itashukua mkondo wake .
 Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanga akizungumza na waandishi wa habari juu ya utata wa mgombea Urais, Wallace Karia  leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanga leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad