HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 24 August 2017

HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE YAPATA NAIBU MEYA MPYA


Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akizungumza wakati wa 
kikao cha baraza la madiwani wakati wa kufanya uchaguzi wa Naibu Meya  ambapo kisheria kila mwaka hupatikana Naibu Meya mpya. 
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepata Naibu Meya mpya, katika kikao cha baraza la madiwani ambapo kisheria kila mwaka hupatikana Naibu Meya mpya. 

Katika uchaguzi huo kulikua na wagombea wawili ambapo diwani wa kata ya Changombe 
Benjamini Ndalichako akichuana na 
diwani wa kata ya kurasini 

Rajab Mkenga 


Ambapo katika kinyangiro hicho Rajabu Mkenga aliibuka mshindi kwa kura 18 kati ya kura 29 kati ya kura zilizopigwa,huku mpinzani wake akiwa na kura 11. 

Mara baada ya kupata ushindi huo Mkenga aliwashukuru wapiga kura wote na kuwaomba washirikiane katika kuijenga Temeke mpya. 

Pia katika baraza hilo ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa kamati mbalimbali ambazo zitashirikiana katika mambo ya kijamii na maendeleo ya Temeke, kamati hizo ni pamoja na kamati ya uchumi na uongozi, kamati ya mipango miji, kamati ya Afya Elimu na Uchumi,Kamati ya nidhamu na maadili, Kamati ya Fedha na uongozi na kamati ya kugawa Ardhi.
Madiwani wakiwa wanafuatilia 
kikao cha baraza la madiwani wakati wa kufanya uchaguzi wa Naibu Meya  ambapo kisheria kila mwaka hupatikana Naibu Meya mpya. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad