HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 21 August 2017

MKE WA RAIS MUGABE AREJEA ZIMBAMWE KIMYA KIMYA BAADA YA KUKUMBWA NA TUHUMA ZA KUMJERUHI MTU AFRIKA KUSINI

Mke wa rais wa Zimbabwe, Garce Mugabe amerejea nchini Zimbabwe akitokea Afrika Kusini licha ya tuhuma za kumdhuru mwanamke mmoja kwenye hoteli Jijini Johannerburg.

Grace Mugabe mwenye umri wa miaka 52, amewasili Jijini Harare mapema leo kwa mujibu wa radio moja ya Zimbabwe, licha ya kuwepo kwa jitihada za kumzuia Afrika Kusini.
Mwanamitindo Gabriella Engels akiwa na plasta kichwani katika eneo aliloumia baada ya kupigwa na Grace Mugabe

Grace alikuwa anapaswa kuhudhuria mkutano siku ya jumamosi nchini Afrika Kusini lakini hakutokeza. Pia inadaiwa aliomba kupatiwa kinga ya Kidiplomasia.

Mama Mugabe anatuhumiwa kumpiga kwa waya wa umeme mwanamke mmoja mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 kichwani na kumjeruhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad