HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 6 August 2017

Dkt. Ashatu Kijaji : UTT Microfinance ni mfano wa kuigwa na taasisi za kifedha

Na Mwandishi wetu, Dodoma
Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC imetakiwa kuendelea kuwa mfano wa kuingwa na taasisi zingine za kifedha katika kuviwezesha vikundi vya kijasiriamali na saccos ili kuchocheo vipato vya wananchi na ukuaji wa uchumi wa nchi hasa katika azma ya kufikia uchumi wa viwanda. 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alisema hayo wakati wa ziara yake ya kujionea utendaji wa taasisi hiyo na shughuli za kijasiriamali zilizonufaika na mikopo toka taasisi hiyo mjini  Dodoma, kuwa inahitajika kuendelea kufanya kazi nzuri na taasisi zingine ziige mfano huo. 

“Katika ziara yangu nimeona taasisi ya UTT Microfinance inafanya kazi nzuri ya kuwezesha wananchi hadi vijijini,” moja ya jambo kubwa ni kwamba imewezesha vikundi vya wajasiriamali na Lubala Saccos kupata mikopo nafuu, aliongeza kusema,Dkt.Kijaji.

Lubala Saccos ilipatiwa mkopo na taasisi hiyo na Bebki ya TIB na imeweza kuwa na shamba  la ekari 170 la zao la Zabibu na inaundwa na wanachama 103 toka vijiji vya vitatu vya kata ya Lamaiti yaani Lukali, Bankolo na Lamaiti yenyewe Wilayani Bahi.

Dkt.Kijaji alisema wakati umefika kwa taasisi za kifedha kutoka mjini na kwenda kuwatafuta wananchi vijijini na kuwapatia mitaji waanzishe miradi ya ujasiriamali na hiyo itaongeza ajira na kupunguza wimbi la vijana kukimbilia mjini.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo ya UTT Microfinance PLC,Bw. James Washima alisema taasisi hiyo inaendelea kufanya vizuri ya utoaji wa huduma za kifedha kwa wananchi na itahakikisha inazidi kujipanua katika huduma zake hadi maeneo mengi ya vijijini.

“Tunatekeleza sera ya serikali ya kuwezesah wananchi kiuchumi hususani wenye kipato cha chini na kati kwa kuwapatia mikopo” na wataendelea kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa ili wananchi wapate fursa za kuanzisha miradi kijasiriamali,aliongeza kusema Bw. Washima. 

Pia alisema ili kuleta ufanisi katika sekta ndogo ya kifedha, kunahitaji kuwepo kwa sheria itakayosimamia shughuli za utoaji mikopo tofauti na ilivyo hivisasa ambapo kuna sera lakini hakuna sheria ya kusimamia.

Alifafanua kwamba kutokana na mazingira hayo wakopaji wengi wamekuwa wakijikuta mali zao zikipigwa mnada sababu hakuna sheria ya kusimamia eneo hilo na kwa kufanya hivyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi.

Bw. Washima alisema benki yake  inamatawi 12 Tanzania Bara na Zanzibar na vituo 46 vya kutoa huduma karibu na watanzania.

Naye Diwani wa Kata ya Lamaiti Wilani Bahi, Bw. Donald Mejitii alisema  Lubala saccos inamiliki shamba lenye ekari 200, na tayari imelima zao la zabibu katika ekari 170 na wanataraji itaongeza kipato cha wanachama wake.

 “Lubala saccoss ilipata mkopo toka taasisi ya UTT Microfinance na taasisi zingine kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na uandaaji wa shamba na sasa zao limeaza kuzaa,” na wanataraji hapo baadaye kujenga kiwanda cha kusindika zao hilo, alifafanua Diwani huyo.

Alisema shamba linatazamiwa kuzalisha tani 4500 ya zabibu kwa mwaka zenye ubora wa kiwango kizuri. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) akizungumza jambo wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo, Profesa Godwin Mjema na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. James Washima.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji aliyesimama akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali Mkoani Dodoma walionufaika na mikopo toka Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC, kulia kwake wa kwanza ni Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo,Profesa Godwin Mjema na wa pili ni Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. James Washima.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji mbele akiangalia zao la zabibu katika shamba la ekari 170 linalomilikiwa na Lubala Saccos katika kijiji cha Lamaiti Wilayani Bahi ambalo limenufaika mkopo toka Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC, wa pili kulia mwenye fulana ni Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo, Profesa Godwin Mjema na wa kwanza kulia mwenye kofia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. James Washima, watatu toka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi. Elizabeth Kitundu na wapili kushoto ni Diwani wa Kata ya Lamaiti,Bw. Donald Mejitii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad