HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 31 August 2017

CHUO CHA USAFIRI WA ANGA CATC, KINACHOMILIKIWA NA TCAA CHATUNUKIWA TENA CHETI CHA TRAINAIR PLUS

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari,(Kushoto) akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kinachomilikiwa na TCAA, katika hafla fupi ya kupokea Cheti Trainair Plus ambacho kinatambua Chuo cha CATC kama  Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Hamza S. Johari(Kushoto) akimsikiliza  Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kinachomilikiwa na TCAA, Aristide Kanje(Kulia) katika hafla fupi ya kupokea Cheti chaTrainair Plus, ambacho kinatambua Chuo cha CATC kama Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza S. Johari (Kati kati)na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kinachomilikiwa na TCAA, Aristide Kanje(Kulia) Wakifurahia Cheti  cha Trainair Plus kinachotambua CATC kama Mwanachama Shirikishi  wa Shirikisho la Umoja wa Vyuo Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). 
Mkurgenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari (Kati Kati) Akionyesha  Cheti cha Trainair Plus Kilichotunukiwa kwa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Kinachomilikiwa  na TCAA. CATC Imefuzu kuwa  Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Watumishi wa Chuo Cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) wakifurahia kutunukiwa Cheti cha Trainair Plus. CATC imetunukiwa Cheti hicho baada ya kufuzu kuwa  Mwanachama shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). 
Mkurgenzi Mkuu,Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari (Kati Kati) Akifungua Cheti cha Trainair Plus Kilichotunukiwa kwa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Kinachomilikiwa  na TCAA. CATC Imefuzu kuwa  Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). 

Kwa mara nyingine  Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania( CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kimefuzu na kutunukiwa cheti cha kuwa  mwanachama Shirikishi wa wa Umoja wa Vyuo Vya Mafunzo ya Usafiri wa Anga Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Cheti hicho ambacho maarufu kama TrainAir Plus, kimetolewa na Shirikisho la  TrainAir Plus, wiki hii baada ya CATC kufuzu vigezo na masharti ikiwa ni pamoja na kuandaa mitaala inayokubalika na shirikisho. Kwa mara ya kwanza CATC ilitunukiwa cheti hicho mwaka 2012 na muda wake uliisha mwaka 2015.
Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza S. Johari amewachagiza watumishi wa chuo cha CATC kufanya kazi kwa bidiii na kuhakikisha CATC inaendelea kujiimarisha  na kutoa mafunzo  bora zaidi.
Hiki ni chuo cha kimataifa kwa kuwa kinatoa mafunzo  kwa wanafunzi wa  kutoka nje ya nchi,  lengo letu tuhakikishe tunakuwa wanachama kamili wa TrainAir Plus, Amesema Hamza . Ameahidi kutoa msaada unaohitajika katika kukiimalisha chuo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa  Chuo cha CATC, Aristide Kanje, Amemuhakikishia Mkurugenzi Mkuu kuwa timu yake itaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha chuo hicho  kinatakeleza majukumu yake kama inavyotakiwa.
Pamoja na faida nyingine, vyuo wanachama  wa TRAINAIR PLUS wana fursa ya chuo kutambulika kimataifa,  kupata, kubadilishana  mitaala ya masomo  ya usafiri wa anga inayoandaliwa kwa kufuata viwango vinavyokubalika kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad