HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 15, 2017

BENKI YA EXIM YATOA MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO 40 KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE.

Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni zawadi kwa hospitali hiyo kwa kujali jamii na kusheherekea miaka 20 ya Benki ya Exim Tanzania. 
 Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda akizungumza katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam leo wakati wakisheherekea miaka 20 ya benki ya Exim Tanzania pamoja na kutoa msaada wa Vitanda na Magodoro 40 katika hospitali hiyo ikiwa benki hiyo inaijali jamii. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Matawi ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu. Na kutoka Kulia ni Katibu wa Afya, Sanura Kondo na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi(Katikati) akiwashukuru Benki ya Exim mara baada ya kutoa msaada wa Magodoro na Vitanda 40 katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni  Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda na Kulia ni
Katibu wa Afya, Sanura Kondo na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi.

BENKI ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 katika hospitali ya Wilaya ya Temeke ikiwa ni shukrani yao katika kuadhimisha miaka 20 ya Benki hiyo ya kujali jamii ambapo msaada huo utawekeza shilingi milioni 200 katika sekta ya afya Tanzania. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda wakati wa kuwakabidhi vitanda 40 katika hospitali ya wilaya ya Temke jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa
 Mradi huu unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini hivyo benki ya Exim itatoa magodoro 500 na vitanda katika hospitali za serikali mikoa 13 nchini.

 “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.” amesema Ponda.
 Nae 
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke Dkt. Husna Msangi amesema,kuwa  “ Upungufu wa vitanda katika hospitali ya Tememke ni changamoto kubwa. Tunahitaji vitanda  katika wodi ya watoto na wodi ya wazazi. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii katika hospitali yetu.”

Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali, katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Mtwara, Pemba na Unguja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad