HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 1 August 2017

BENKI YA CRDB YAKABIDHI GARI KWA KITUO CHA POLISI KAWE, JIJINI DAR LEO

Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa (wa pili kulia) akikabidhi funguo ya gari mpya aina ya Toyota Land Cruser kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni aliyehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo Kitengo cha Mafao na Fidia, SACP Suzan Kaganda (wa nne kushoto) ikiwa ni makabidhiano ya gari la kusaidia doria kwa Kituo cha Polisi Kawe, Jijini Dar es salaam. Gari hilo lenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 70, limetolewa na Benki ya CRDB kwa kituo hicho. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika mchana wa leo katika Kituo cha Kawe jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni Kamanda wa Polisi wa Kinondoni wa sasa, ACP Murilo Jumanne Murilo, Afisa Mtendaji Kata ya Kawe, Husna Nond, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, OCD Jackson Simba pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi Kawe, ASP Samson Mwambungu. 
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla ya kukabidhi gari kwa Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, jijini Dar es salaam.
Kamanda wa zamani wa Polisi Mkoa wa Kinondoni aliyehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo Kitengo cha Mafao na Fidia, SACP Suzan Kaganda akizungumza katika hafla ya kukabidhi gari kwa Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Godwin Semunyu akiongoza hafla hiyo.
Meza kuu.
Ujumbe wa Benki ya CRDB ukiongozwa na Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa ukiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Kipolisi ya Kawe pamoja na wadau wengine.
Kamanda wa zamani wa Polisi Mkoa wa Kinondoni aliyehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi hiyo Kitengo cha Mafao na Fidia, SACP Suzan Kaganda akiendesha gari hilo baada ya kukabidhiwa, huku Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akifurahia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoani wa Kinondoni, ACP Murilo Jumanne Murilo (katikati) akizungumza baada ya kukabidhiwa gari na kabla ya kulikabidhi kwa OCD wa Wilaya ya Kinondoni, OCD Jackson Simba (kushoto).
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad