HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 10, 2017

ZOEZI LA KUOROZESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI KUANZA KESHO

Na Veronica Kazimoto 
WADADISI wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 wameaswa kuzingatia maadili ya kazi wakati wa zoezi la kuorozesha kaya linalotarajia kuanza kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utafiti huo.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa wadadisi hao, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema ili kufanikisha zoezi la uorodheshaji wa kaya, ni lazima wadadisi hao wakazingatia maadili ya kazi pamoja na kufuata taratibu zote za Utumishi wa Umma.

“Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawaagiza kwenda kwenye jamii kwa ajili ya kuorodhesha kaya zitakazofanyiwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Natumaini mtatii na kuheshimu maadili ya Utumishi wa Umma ili muweze kufanikisha kazi hii kwa ufanisi,” amesema Slyvia Meku.

Amesema Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya litafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa takribani siku 15 kuanzia kesho Julai 11, 2017 na baadae kufuatiwa na utafiti wenyewe unaotarajia kuanza mwezi Desemba, 2017.

Sylvia Meku amesema utafiti huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuangalia kiwango cha umasikini nchini. 
 Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku akizungumza wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
  Baadhi ya Wadadisi wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku (hayupo Pichani) wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
Baadhi ya Wadadisi wakiwa kwenye gari wakielekea Kata ya Mchikichini, Ilala na Kawe jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
 Baadhi ya Wadadisi wakielekezwa namna ya kutumia ramani wakati wa kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo na Mtalaam wa Ramani Jumanne Msuya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad