HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 10 July 2017

WILLIAM NGELEJA ARUDISHA PESA ZA ESCROW

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amesema katika kipindi cha zaidi ya miaka 12 akiwa kiongozi wa umma hakuwahi kukumbwa na kashfa yoyote ya rushwa na ufisadi.
Ameyasema hayo leo Jumatatu, Julai 10 wakati akitangaza uamuzi wake wa kurudisha Sh 40.4 milioni fedha za mgawo wa Escrow alizozipokea kutoka kwa mfanyabiashara James Rugemalira.
Amesema amerudisha fedha hizo kwa kuwa amesononeka na kufadhaika baada ya kuona msaada aliopewa unahusishwa na tuhuma.
Kuhusu kuchelewa kurudisha fedha hizo baada ya Rugemalira kutuhumiwa, Ngeleja amesema alishindwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa haikuthibitishwa kama mfanyabiashara huyo ana kashfa.


Mbunge wa Sengerema Mh. William Ngeleja (kushoto) akionesha nakala ya malipo ya kiasi cha shilingi milioni 40.4 alizozirejesha Serikalini (TRA) fedha alizopewa kama msaada toka kwa Bw. James Rugemalira wa Kampuni ya VIP Engeneering and Marketing Ltd, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Mbunge wa Sengerema Mh. William Ngeleja (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kurejesha kiasi cha shilingi milioni 40.4 Serikalini (TRA) fedha alizopewa kama msaada toka kwa Bw. James Rugemalira wa Kampuni ya VIP Engeneering and Marketing Ltd, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa. Picha zote na Eliphace Marawa – Maelezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad