HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 28 July 2017

WAZIRI MAKAMBA ATOA RAI KWA WAANDAAJI WA MICHUANO YA NDONDO CUP

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Janury Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa michuano hiyo (katikati) Shafii Dauda na Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kisongo.


Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Janury Makamba jana akiwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza ya michuano ya Ndondo Cup 2017 kwenye uwanja wa Kinesi-Sinza.
Wakati akitoa neno baada ya mchezo kati ya Vijana Rangers vs Kibada One,  Makamba amezungumzia changamoto nne ambazo zinatakiwa kutatuliwa ili kupiga hatua kwenye soka la Tanzania.
“Changamoto kubwa ni kuendeleza mashindano haya lakini kuendeleza soka la Tanzania, mpira unahitaji vitu vinne ili ufanikiwe. Kwanza unahitaji vipaji ambavyo vipo, pili miundo mbinu ya mchezo wenyewe kama viwanja, academies na kadhalika, tatu tunahitaji mifumo ya kuvumbua na kuendeleza vipaji lakini naamini mashindano haya yanatoa fursa hiyo ya kuvumbua na kuviendeleza halafu tunahitaji utawala ‘sports management’,”
“Nimeshuhudia mpira mzuri sana ambao ulikuwa na ushindani mzuri na nguvu sawa ndio maana mshindi amepatikana kwa penati. Kubwa zaidi nimeshuhudia mwamko mkubwa sana lakini tunaona mafanikio makubwa kwenye mashindano haya ya Ndondo Cup na wote waliohudhuria hapa wamepata burudani.”
 Makamba amesema amefurahi kuwa karibu na wananchi alipokwenda kushuhudia mechi ya Ndondo tofauti na anapokwenda kwenye mechi nyingine ambazo ni rasmi sana ambapo huwa na itifaki kubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad