HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 27 July 2017

WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE

Na Agness Francis wa Globu ya Jamii
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amewatia mbaroni wahalifu wa makundi ya ukabaji na uporaji  nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
Vibaka hao wanaoshikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa  umri wao ni kati ya miaka 12-25, opresheni hiyo ilikamata wahalifu 8 kutoka Mbande na wengine 8 kutoka Chamazi wilayani humo.
Hata hivyo waalifu hao walikiri kuwa makundi na vishawishi ndio huwafanya kupelekea kufanya matukio hayo kwa kutumia visu na mapanga kwa kupora pochi za kina mama  kuchukua simu pamoja na fedha.
Vile vile alikemea utoro wa wanafunzi   na kutaka wazazi kurejeshe watoto mashuleni na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya msingi katika kupata elimu.
Nae mzazi Zuhura Hamza alizungumza` kwa kusema watoto wenyewe ndio hawasikii hawataki kusoma wamejitahidi kadri ya uwezo wao lakini hawajapata suluhu la tatizo hilo hivyo akiomba msaada kwa wakuu wa shule.
Kamanda Muruto  alitoa wito kwa wazazi wawahimize watoto kwenda shule, kwani watoto wamezagaa mitaani na kujiingiza katika makundi mabovu  kama ya madawa ya kuevya, uporaji, uvuataji bangi na sigara.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo picha) kuhusu kuwashikilia watuhumiwa wa makundi ukabaji na uporaji nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja na  wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto akiwaonesha wanahabari watuhumiwa wa makosa mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad