HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 21 July 2017

WATAALAM WA USAFIRI WA ANGA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WATUMIAJI WA USAFIRI WA ANGA

Wataalam wa Usafiri wa Anga  nchini wamekutana katika semina ya siku tatu ya kuwajengea uwezo kuhusu namna bora ya kushughulikia malalamiko na kero za watumiaji wa usafiri wa anga nchini katika semina iliyofanyika mjini Morogoro kuanzia  Julai 20, 2017. 
Semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  nchini imewakutanisha wajumbe wa kitengo cha Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga cha TCAA(TCAA-CCU), Watendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC), wanasheria wa Mamlaka na maafisa  kutoka idara ya udhibiti masuala ya Kiuchumi ya TCAA ambayo inajukumu la kulinda maslahi ya watumiaji wa usafiri  wa anga .
Miongoni mwa mada zilizotolewa kwenye semina hiyo ni pamoja na  wajibu wa  kampuni za ndege kwa abiria, iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa  TCAA, Hamza S. Johari, majukumu ya kitengo cha kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga na  nyezo za kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga.
Semina hii ni sehemu ya mkakati wa usafiri wa anga wa kuboresha huduma zinazotolewa kwa watumiaji wa usafiri wa anga na kukuza sekta ya usafiri wa anga Tanzania
 Mkurugenzi  Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari, akitoa mada kuhusu wajibu wa Mashirika ya Ndege kwa Abiria Kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu Kuhusu Namna ya Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga Nchini Iliyofanyika Morogoro, Kuanzia Julai 20, 2017. 
 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kudhibiti Masuala ya Kiuchumi, Dan Malanga wakifuatilia mada kwenye semina kuhusu namna ya kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Morogoro Mwezi July 20, 2017.
 Washiriki wa Semina kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya matumiaji wa Usafiri wa Anga wakifuatilia mada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC) Elias Mwashiuya, akiwasilisha mada kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Morogoro Julai 20, 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad