HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 20, 2017

UHAMISHO WA WATUMISHI WA UMMA UFANYIKE KWA MAKINI

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Segerea alipofanya ziara ya kikazi  ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo akiwatambulisha baadhi ya watumishi na viongozi wa Segerea waliohudhuria kikao kazi kilichowakutanisha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko kutoka kampuni ya Watumishi (Watumishi Housing Company), Bw. Raphael Mwabuponde, akiwasilisha mada kuhusu taratibu za kupata nyumba kwa Watumishi wa Umma wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na Watumishi wa Umma wa Segerea, Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mhe. Bonnah Kaluwa akitoa salamu wakati wa kikao kazi na kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), leo Jijini Dar es Salaam.  
 Mkazi wa Segerea, Bw. Juma Kali akiwasilisha hoja maalum wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala - Segerea  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa Umma kutoka Tabora, Bw. John Joseph akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kutoka Segerea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amezitaka Taasisi za Serikali kuratibu suala la uhamisho wa watumishi wa umma kwa makini pale inapohitajika kufanya hivyo Ili kuepuka kero na usumbufu kwa watumishi. 

Waziri Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema uhamisho lazima ufanyike kwa mtumishi wa umma endapo kukiwa na sababu za msingi sana. “Naomba ieleweke kuwa uhamisho una taratibu zake hivyo kila mwajiri ni mwajiri akazifuata.” Mhe. Kairuki alisisitiza.

Ameongeza kuwa imebainika wapo baadhi ya watumishi wa umma wanawasilisha sababu mbalimbali kwa waajiri kuomba kuhama wakiwa na nia ya kukwepa kukaguliwa sifa zao za elimu. 

Waziri Kairuki amesisitiza kuwa uhamisho usifanyike kwa mtumishi ambaye anaonekana kuwa na matatizo.

“Baadhi ya waajiri wamekuwa na tabia ya kuwahamisha watumishi wa umma ambao wameonekana kuwa na tatizo na kuwahamishia sehemu nyingine, uhamisho wa namna hii haukubaliki, tatizo la mtumishi linatakiwa kufanyiwa kazi kwenye kituo chake cha kazi na sio kupeleka tatizo sehemu nyingine.” Mhe. Kairuki ameongeza.

Mhe. Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama ambapo leo ni siku ya tisa akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala-Segerea kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.

Waziri Kairuki katika vikao kazi amehimiza watumishi wa umma nchini kubadili mtindo wa maisha, kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi, kujiepusha na ugonjwa wa UKIMWI, na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY). 

Lengo la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad