HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 5 July 2017

UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA WAVU WASOGEZWA MBELE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

UCHAGUZI wa Chama cha Mpira wa Wavu Nchini umesogezwa mbele mpaka Agosti 13 ili kutoa nafasi kwa vyama vya mpira huo mikoani kupata viongozi wake.

Awali uchaguzi huo ulitakiw aufanyike Julai 8 mwaka huu umeweza kusogezwa mbele na Baraza la Michezo Taifa (BMT) ili kuwapa nafasi vyama vya mikoa kumaliza chaguzi zao za viongozi wa mikoa ili kwenda katika uchaguzi mkuu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na BMT huku ikisisitiza vyama vya mikoa kufanya chaguzi zao kwa wakati pia kamati za michezo za mikoa kusimamia chaguzi zote za chama za mpira wa  wavu katika mikoa yao.

BMT imevitaka vyama vya mpira wa wavu vya mikoa ambavyo vimesajiliwa katika mikoa yao vihakikishe vinafanya uchaguzi kwa wakati ili viweze kupata haki ya kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma ukiwa ni uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi watakaosimamia mpira wa wavu nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad