Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA ) imetoa msaada vifaa mbambali katika kituo cha afya cha Magomeni ambavyo vilitelekezwa kutokana na kodi.
Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Huduma wa Elimu ya Mlipakodi, Valentina Baltazar amesema kuwa kutokana na sheria Kamishina Mkuu ana mamlaka ya kutoa vitu vilivyotelekezwa kwa ajili ya kusaidia jamii .
Amesema vifaa hivyo vina zaidi ya miaka mitano vipo katika ghala ya ubungo vikiwa vimetelekezwa kutokana na kushindwa kulipiwa kodi na mtu aliyekuwa ameviagiza.
Valentina amesema kuwa Kituo cha Afya Magomeni waliomba vifaa hivyo katika mamlaka na kujiridhisha na maombi ya kutoa vifaa hivyo kwa ajili kusaidia wananchi.
Nae Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magomeni ,Dk. Faith Mdee amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana ambao utakwenda kusaidia hata hospitali ya Mwananyamala.
Amesema baada ya kupoke vifaa hivyo sasa changamoto iliyobaki kwao ni gari la kubeba wagonjwa ambapo wameoimba TRA kama wa magari waweze kuwasiadia.
Meneja wa Huduma wa Elimu ya Mlipakodi wa TRA, Valentina Baltazar akizungumza na waandishi habari mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali katika Kituo cha Afya cha Magomeni.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magomeni ,Dk. Faith Mdee akizungumza na waandishi habari juu ya msaada katika kituo cha afya cha Magomeni.
Meneja wa Huduma wa Elimu ya Mlipakodi wa TRA, Valentina Baltazar akimkabidhi moja kitanda cha wagonjwa kwa Muuguzi Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magomeni , Upendo Mkuluma jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya nguo mbalimbali za msaada katika Kituo cha Afya Magomeni.
No comments:
Post a Comment