HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 14 July 2017

TIRA:YEYOTE ATAKAYEKAMATWA NA BIMA FEKI SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE

Mwanasheria Arthur Mbena kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) akiwa katika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. sabasaba jijini Dar es salaam.Picha na Vero Ignatus Blog. 
Bango la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini lenye maelezo namna ya kutambua bima kama ni halali au ni feki kama maelezo yanavyosomeka hapo .Picha na Vero Ignatus Blog 
Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Arthur Mbena akiwana Paul Abdiel ambae ni Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA)Makao makuu Dar es salaam wakiwa katika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. Picha Vero Ignatus Blog.
Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Arthur Mbena akiwana Paul Abdiel ambae ni Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA)Makao makuu Dar es salaam wakiwa katika maonyesho yakatika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. wakiwa wanatoa elimu kwa mteja aliyetembelea banda hilo katika maonyesho haya.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na,Vero Ignatus Dar es salaam. 
Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini( TIRA)imetoa rai kwa wananchi kutumia mfumo wa TIRA MIS ambao utamsaidia mteja kutambua bima za vyombo vya moto zenye uhalali au feki kwa kutumia mfumo wa kieletroniki. 

Hayo yamesemwa na mwanasheria Arthur Mbena ambapo amesema kuwa mtu yeyote yule ambae atakamatwa na bima feki sheria itafuata mkondo wake, ameainisha njia ambazo mtu anaweza kutambua bima yake kama ni feki ama halali kwa kutumia simu ya mkononi( smart phone)kutumia mtandao http/mis.tira.go.tz,google unadownlod tira mis.

Aidha amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini ni kuwa msimamizi wa sekta ya Bima mwenye kiwango kinachokubalika Kimataifa,kuendeleza ,kukuza masoko ya Bima imara,shirikishi lenye kuthamini usawa na utendaji mahiri,kwa manufaa na kulinda maslahi ya wateja.
Kwa upande wake Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA) Paul Abdiel amesema kuwa mamlaka hiyo inafanya shughuli zake kwa weledi, kuwapa kipaumbele wateja ,ushirikiano ,kuwajibika, pamoja na kuaminika na uwazi 

Amewataka wateja wa Bima za vyombo vya moto kuwa makini pale wanapokatiwa Bima hizo wazihakiki na kuhakikisha kama ni halali ama la.
Wananchi wakiwa wanaingia katika banda la Wizara ya Maliasili na utralii kama inavyoonekana pichani .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wananchi kama inavyoonekana pichani wakiwa katika maonyesho hayo ya 41 ya Biashara ya Kimataifa sabasaba .Picha na Vero Ignatus blog 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad