HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 July 2017

TANROADS MOROGORO NA RUKWA WAPONGEZWA.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wananchi wa kijiji cha Kilosa kwa Mpembo, wakati alipokagua ukarabari wa barabara ya Lupilo -Lumecha kupitia Kilosa kwa mpembo hadi Londo yenye urefu wa kilomita 220.5.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin ngonyani (wa pili kushoto) akikagua barabara ya kutoka Kilosa kwa mpembo hadi Londo ambayo imetobolowa na kukamilika na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Wa tatu kulia ni Mbunge wa Malinyi Dkt. Haji Mponda. .
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Mbele) akipita kwenda kuangalia maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Ruhuhu, wakati alipokagua ujenzi wake Mkoani Ruvuma. Wa pili Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoani Ruvuma Eng. Razack Alinanuswe.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Mahenge akisistiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake.
Mhandisi Mkazi Eng. Napegwa Kiseko akimweleza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani ( wa tatu kushoto) hatua iliyofikiwa ya Ujenzi wa Daraja la Ruhuhu, wakati Naibu Waziri huyo alipokagua hatua za ujenzi wake Mkoani Ruvuma. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani ameupongeza uongozi wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Morogoro na Ruvuma kwa kutekeleza agizo alilowapa la kufanya matengenezo barabara ya Lupilo -Lumecha kupitia Kilosa kwa mpembo hadi Londo yenye urefu wa kilomita 220.5. na kuweza kupitika kwa magari yenye uwezo mkubwa. 

Ametoa pongezi hizo wakati akikagua barabara hiyo ambapo amesema kutengenezwa kwake kutawezesha magari yenye uwezo mkubwa kupita na kufungua mawasiliano baina ya Wilaya ya Malinyi iliyopo mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Namtumbo iliyopo mkoa wa Ruvuma. 

“Niwapongeze TANROADS kwa kutoboa barabara hii na kuwezesha baadhi ya magari kuweza kupita kama Mimi nilivyopita kwa mara ya kwanza kuelekea wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma kwa kutokea Morogoro,” amesisitiza Eng. Ngonyani. 

Ameongeza kuwa barabara hiyo imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na hatua inayofuta ni kitangaza zabuni ili iwekwe katika mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami. 

“Barabara hii iliahidiwa kujengwa kwa lami kwa awamu tofauti tofauti za uongozi, na Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kukamilisha ahadi hii Ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kufungua fursa za mawasiliano baina ya upande hizi mbili,” amesisitiza Eng Ngonyani. 

Naye Mbunge wa Malinyi Mhe. Dkt. Abdalla Mponda ameishukuru serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu Kufanya matengenezo na kuitoboa barabara hiyo na kufufua matumaini ya wananchi wa Malinyi na wilaya ya Namtumbo. 

Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amekagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mto Ruhuhu na kumtaka mkandarasi wa kampuni ya Lukolo Co.ltd kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo unakamilika kwa wakati ili lianze kutumiwa na wananchi. 

“Nataka kuona Daraja hili linakamilika mapema, ili kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wa wilaya Nyasa na Ludewa wananchi hawa wamekuwa wakitumia kivuko ambacho kimekuwa kikitumika kwa miezi minne kwa mwaka na wakati wa mvua kubwa hakiwezi kutumika,” amesema Eng. Ngonyani. 

Kwa Upande wake Mkandarasi Kutoka Kampuni ya M/s Lukolo Company Limited, Mhandisi Maulid Annesye amemuhakikishia Eng. Ngonyani kuwa wataongeza kasi ya ujenzi kwani wamepata vifaa vya kutosha ili kuukamilisha mradi huo. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amemaliza Ziara yake ya siku mbili Mkoani Ruvuma ambapo amekagua miundombinu ya Barabara na vivuko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad