HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 29, 2017

RC MAKONDA AKABIDHIWA RIPOTI YA WEZI NA MAGARI NA VIFAA DAR, 73 MBARONI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa ripoti ya wezi wa magari pamoja na vifaa vya magari vya wizi na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam DCP Lucas Mkondya ikiwa ni wiki mbili toka mkuu huyo aliagize jeshi hilo kuchukua hatua baada ya matukio ya namna hiyo kushamiri ndani ya mkoa huo. 
 Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi hii wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda Mkondya alisema katika operesheni hiyo kali jumla ya wahumiwa 73 wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, power windows, radio, injector pumps, starters na seat cover. 
 “Tarehe 19 mwezi wa saba mweshimiwa RC Makonda ulitoa maagizo kwa jeshi la polisi kwamba unatupatia siku saba kuhakikisha tunasambaratisha mtandao wa wezi wa vifaa vya magari pamoja na magari baada na sisi tumelitekeleza hilo tayari kuna watu 73 tunawashikilia
"Kinondani wamekamatwa watuhumiwa 29, Ilala wamekamatwa wahutumiwa 33 na mkoa wa kipolisi Temeke wamekamatwa wahumiwa 11,” alisema.
Alieleza kuwa  jumla ya power windows zilizokamatwa ni 40, Radio 12, Taa za magari aina mbalimbali 105, side mirrors 92, vitasa vya magari 109, wiper switch 7, Tampa 4, left pump3, Air cleaner 1, Booster 3, show grill 6, machine za kupandisha vioo 1 na tyre used 2. 
 Pia alisema katika mahojiano na wahutumiwa wote waliokamatwa wapo walioshindwa kuvitolea maelezo vifaa hivyo ni namna gani na wapi wamevipata, na wote  wanaendelea na mahojiano na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao wote unaojihusisha na wizi huo wa vifaa vya magari ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahamani kwa hatua zaidi. 
 Kwa upande wa RC Makonda alisema yeye anataka kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa salama ili kutimiza gamma ya Rais John Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi wake.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wanahabari leo wakati akikabidhiwa ripoti ya wezi wa vifaa vya magari.
 Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam DCP Lucas Mkondya akizungumza na wanahabari juu ya watuhumiwa 73 ambao wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akikagua vifaa vya magari vinavyosadikiwa kuwa ni vya wizi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akikagua vifaa vya magari vinavyosadikiwa kuwa ni vya wizi leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya vifaa vya magari vinavyosadikiwa kuwa ni vya wizi vilivyooneshwa na jeshi la polisi leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad