HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 16 July 2017

Rais Magufuli aomboleza kifo cha mke wa Dk Mwakyembe

Rais John Magufuli, amemtumia rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kutokana na kifo cha mkewe Linah kilichotokea usiku wa Julai 15.
Linah amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa ya Ikulu imesema, Rais Magufuli ameeleza kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho.
Amsema pamoja na familia yake wanaungana na Dk Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Nakupa pole sana Dk Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,” amesema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad