HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 22 July 2017

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika Hospitalini hapo, Julai 22, 2017. Wengine pichani ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge (katikati), Mjumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Sarah Mwaga (wa pili kulia) pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Caroline Damian. Mfuko huo umetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 99 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula (wa nne kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) wakiangalia moja ya vitanda vya kujifungulia wakina mama, vilivyotolewa na Mfuko huo, kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017. 
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Samuel Seseja akizungumza machache katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.
Sehemu ya washiriki katika hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi Kadi ya Uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama Mkoa wa Dodoma, Dkt. Leah Kitundya, katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi Kadi ya Uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Dodoma, Dkt. Caroline Damian, katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akipokea cheki cha shukrani kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Sarah Mwaga, kwa mchango wao waliutoa kwa Hospitali hiyo.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakijiandikisha kwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF.Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akiwajulia hali wakina mama waliolazwa katika wadi ya wazazi, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad